Kiislamu vyanzo

  1. home

  2. article

  3. Uislamu Chaguo Langu 10 + Sauti

Uislamu Chaguo Langu 10 + Sauti

Rate this post

Sikiliza

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika kipindi hiki kinachowaangazia watu ambao baada ya kufanya utafiti wa kina wameamua kufuata njia ya haki na ukamilifu maishani ambayo ni njia ya Uislamu. Kuenea dini tukufu ya Kiislamu ni jambo ambalo linazingatiwa kwa kina na kufanyiwa utafiti. Kila siku tunashuhudia watu wanaotafuta imani ya kweli wakivutiwa na Uislamu. Watu wanaosilimu ni wataalamu katika nyanja mbali mbali zikiwemo kama vile   Sanaa na Fasihi. Leo tutamuangazia Mfaransa aliyesilimu Bi. Claire Jobert. Karibuni kujiunga nami hadi mwisho.

@@@

Claire Jobert ni mzaliwa wa Ufaransa ambaye ana shahada ya kwanza katika taaluma ya malezi na shahada ya uzamili katika fasihi ya watoto.

Mwandishi huyo mtaalamu wa sanaa kutoka Ufaransa anajitahidi kutumia uwezo wake wa kielimu kueneza Uislamu na utulivu katika jamii. Bi. Jobert anautazama Uislamu kwa mtazamo wa ujumla na kusema: “Uislamu ni dini sahali, ya wote, na  isiyo na migongano. Dini hii inaonyesha na kuweka wazi njia iliyojaa nuru. Uislamu ni dini iliyowazi na ambayo imeweka wazi nafasi pana ya mwanaadamu katika maumbile.”

Mtaalamu huyu wa malezi anasisitiza kuwa kuna haja ya kuongoza roho zilizotakasika za watoto kuelekea katika kumuabudu Mungu moja ili wasielekee katika njia potofu. Anaendelea kusema kuwa: “Dini ni harakati ya pande zote yenye lengo la kurekebisha fikra na akida na hivyo kukuza misingi ya juu ya maadili ya mwanaadamu katika kivuli cha kumuamini Mwenyezi Mungu. Dini kwa mafunzo yake sahihi inaweza kuwa chanzo cha ustawi wa kisayansi.

Mfaransa Bi. Claire Jobert anasema hivi kuhusu sababu iliyopelekea asilimu: ‘Wakati ambao nilikuwa nafanya utafiti kuhusu dini na itikadi mbali mbali, niliufahamu Uislamu kwa sadfa. Kabla ya hapo nilikuwa nikidhani kuwa Uislamu, kama Uyahudi ni dini ya kaumu maaulumu na kwa hivyo sikushughulika kufanya utafiti kuhusu Uislamu. Lakini nikiwa katika chuo kikuu mazungumzo ya kidini na kielimu ya wanafunzi kutoka Iran na Lebanon ni jambo ambalo lilinishawishi intake kujua zaidi na hivyo nikaanza kusoma vitabu mbali mbali kuhusu Uislamu. Maudhui iliyonivutia zaidi ni kuhusu uhusiano wa mwanaadamu na Mwenyezi Mungu katika Uislamu na vile vile kuhusu sheria za maisha katika Uislamu.

Baada ya miezi sita ya kujua misingi ya Uislamu  niliamua kuwa lazimia niainishe ni dini ipi nitafuata. Nilikuwa nimeshaona haki na nikaamua kuifuata. Jambo jingine muhimu ambalo lilikua na mchango mkubwa katika uamuzi wangu wa kusilimu ni kutokana na kuwa Uislamu unawakubali na kuwaheshimu Mitume wote wa Mwenyezi Mungu. Kwa hakika ni kupitia Uislamu ndio nilipoweza kumjua vizuri Nabii Issa AS (Yesu). Pamoja na kuwa kutoka utotoni nilikuwa nampenda Nabii Issa lakini sikuweza kuamini yale yaliyokuwa yakifunzwa Makanisani kumhusu. Uislamu uliniwezesha kumtazama Nabii Issa AS kwa matazamo mwingine na kumtambua pia kama Mtume wa Mwenyezi Mungu.”

Mfaransa huyu aliyesilimu anaongeza kuwa: “Baada ya kusilimu nilishuhudia mabadiliko makubwa zaidi katika maisha yangu hasa kuhusu itikadi ya Mwenyezi Mungu. Mtazamo wa Makanisha kuhusu Mwenyezi Mungu si sahihi hata kidogo na ni wa kumchanganya mtu. Suala la mungu baba na mungu mwana si wazi na linahesabiwa kuwa moja ya siri zisizoweza kufahamika katika Makanisa. Baada ya kufahamu mtazamo wa wazi wa Uislamu kuhusu Mwenyezi Mungu nilipata hisia ya kina kuwa nimeufikia ukweli ambao nilikuwa nikiutafuta kwa muda mrefu.”

@@@

Wanawake ni sehemu muhimu ya jamii na wanaweza kuwa na nafasi muhimu katika sekta za kiutamaduni na kisiasa katika jamii.

Kwa kuwataka wanawake wavae vazi kamili yaani Hijabu, Uislamu kwa hakika umeandaa mazingira salama na bora ya wanawake kushiriki katika harakati za kijamii. Aidha Uislamu una sheria zilizojaa hekima kuhusu akhlaqi na maadili ya mwanamke katika jamii ili kuzuia kuenea ufisadi na matatizo mengine yatokanayo na kuchanganyika wanawake na wanaume.

Suala la mwanamke katika Uislamu na nchi za Magharibi ni katika ya maudhui anazozishghulikia Bi. Claire Jobert. Mwanamke huyu Mfaransa aliyesilimu anasema: ‘Wanawake Wafaransa walipata mafanikio katika kupigania haki walizopokonywa katika kipindi chote cha historia lakini pamoja na hayo kuna haki zao nyingi ambazo hawakupewa au walipoteza. Kwa mtazamo wangu tatizo lao ni kuwa lengo lao lilikuwa ni kupata haki kama walizonazo wanaume. Ni kwa sababu hii ndio walishindwa kufikia haki na nafasi yao  ya kipekee katika jamii. Mhanga mkubwa wa harakati hiyo potofu ni familia. Hivi sasa familia inakabiliwa na tishio la kuangamia kutokana na kuwa wanawake na wanaume hawajitazami kama wanaokamilishana bali kila moja anataka kile anachodai ni uhuru binafsi. Kwa hakika katika utamaduni wa sasa wa nchi za Magharibi, mtu binafasi anapewa umuhimu zaidi ya hata familia na ni kwa sababu hii ndio misingi ya familia imedhoofika katika ulimwengu wa Magharibi.

Ufahamu wa nafasi ya mwanamke kama mke na mama  ni jambo ambalo linahitaji kujitolea na subira katika pande zote mbili yaani mume na mke. Lakini kutokana na kuwa katika nchi za Magharibi maslahi ya mtu binafsi yanapewa kipaumbele kuliko familia tunashuhudia kuwa kila panapotokea tatizo ndogo, wengi wanafadhilisha kujiondoa katika ndoa badala ya kuwa na subira. Kutokana na kuwa wanawake wa nchi za Magharibi wametupilia mbali majukumu yao asili, hivi sasa wanatapatapa huku na kule bila kujua nafasi yao katika jamii.”

Bi. Claire Jobert anaendelea kusema kuwa: “Katika kipindi chote cha historia wanawake wamekuwa wakidhulumiwa. Nilikuwa naumia sana kutokana na masaibu hayo ya wanawake na nilifurahi nilipoona katika Uislamu  mwanamke na mwanamume wako sawa kwa mtazamo wa kithamani na sambamba na kuwa wana tafauti katika nafasi na majukumu lakini wanakamilishana.”

Wapenzi wasikilizaji, Hijabu ni chanzo cha uhuru na usalama kwa wanawake katika jamii na wala si kifungo kama inavyodaiwa. Maadui wa Uislamu wamegundua kuwa Hijabu ni silaha ya mwanamke Mwislamu na kwa hivyo katika vita vya vyao vya  kiutamaduni dhidi ya umma wa Kiislamu, eneo wanalolenga sana ni suala la mwanamke. Maadui wanataka kuondoa vazi la Hijab na stara ya mwanamke Mwislamu. Hakuna shaka kuwa maadui wanafahamu iwapo mwanamke Mwislamu atapokonywa stara na vazi la hijab, ufisadi mkubwa utaenea katika jamii za Kiislamu kama ilivyo katika jamii za kimagharibi. Kwa hivyo Wamagharibi kwa kutoa nara potofu na zilizojaa hadaa kama vile usawa na uhuru wa mwanamke wanataka kueneza utamaduni uliojaa ufuska kwa lengo la kuangamiza jamii za Kiislamu. Pamoja na kuwepo njama hizo, aghalabu ya wanawake Waislamu wanasisitiza kuhusu kulinda Hijabu na stara yao.

Bi. Claire Jobert anasema baada ya kusilimu na kuanza kuvaa vazi la Hijab alihisi utulivu wa aina yake. Hivi sasa anaendeleza shughuli zake za kiakademia pasina kuhisi kizingiti chochte na ameandika vitabu kadhaa vya fasihi ya watoto.

Profesa Francis Lamand, Mfaransa mtaalamu wa masuala ya Uislamu anasema hivi kuhusu thamani za juu za Kiislamu: “Uislamu unaweza kuzisaidia nchi za Magharibi kupata njia zilizopoteza. Msingi wa Tauhidi katika Uislamu ni jambo ambalo limepelekea kuendelea kudumu daima harakati za kijamii katika hali ambayo hili haliko tena katika nchi za Magharibi na badala yake tunashuhudia masuala ya kimaada. Njia ambayo nchi za Magharibi zimechukua itapelekea kuangamia jamii na ustaarabu

http://kiswahili.irib.ir