Kiislamu vyanzo

  1. home

  2. book

  3. ABU DHARR

ABU DHARR

ABU DHARR

  • Kikundi cha Wanachuoni Islamic Seminary Publications
  • Dar es Salaam, Tanzania
download

    Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha
Kiingereza, kwa jina la: “Abu Dharr”
Kitabu hiki kinahusu maisha ya Sahaba mkubwa na mashuhuri;
Abu Dharr (Jundab bin Junadah). Abu Dharr alikuwa mtu wa tano
kuingia kwenye Uislamu na upanga wake ulikuwa unafaa sana katika
kuendeleza Uislamu. Aliona mikengeuko mingi katika Uislamu tangu
kuanza kwake, na baada ya kifo cha Mtukufu Mtume mambo
hayakuwa mazuri. Alishuhudia mitafaruku mingi wakati wa
makhalifa watatu wa mwanzo kiasi kwamba hakuweza kuvumilia,
na alianza kukemea maovu yanayofanywa na makhalifa wazi wazi na
kwa ujasiri mkubwa sana mpaka ikafikia Khalifa wa tatu kuchukua
hatua za kumhamisha na kumpeleka jangwani ambako aliishi maisha
ya dhiki mpaka kifo kikamkuta huko.
Kwa bahati mbaya sana wanahistoria wengi wa Kiislamu na wasio wa
Kiislamu hawakuzungumza habari zake kwa kina na kama
inavyostahiki kuwa. Kwa hakika Abu Dharr pamoja na Masahaba
wengine kama vile Amar bin Yasir, Mikidadi, Salman Farsy,
halikadhalika na ami yake Mtukufu Mtume, mzee Abu Twalib na
mke wa Mtume Bibi Khadija, alikuwa ni madhulumu wa historia.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu
wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo
uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo
hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo,
Abudhar final.qxd 7/19/2005 10:54 AM Page E
Taasisi yetu ya ‘Al-Itrah Foundation’ imeona ikitoe kitabu hiki kwa
luhga ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia
Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu, Salman Shou kwa kukubali jukumu hili
la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wote
walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa
kwa kitabu hiki.
Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa
wasomaji wetu na kuzidisha upeo wao wa elimu katika dini.
Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 19701
Dar-es-Salaam.

  • Kikundi cha Wanachuoni Islamic Seminary Publications
  • Dar es Salaam, Tanzania