Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. AL-KASHIF SWAHILI – JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

AL-KASHIF SWAHILI – JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

AL-KASHIF SWAHILI – JUZUU YA ISHIRINI NA NNE

 • Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu hiki kilicho mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi
sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau
Marhum Abu Muhammad wa London.
Kama lilivyo jina la Tafsiri ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo
mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika
fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo.
Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika
vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbalimbali na hivyo kujipatia
wasomaji wengi sana.
Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni
mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana,
kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana
`kwenda na wakati’.
Sifa kubwa ya pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha
sana na kung’ang’ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na
wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo
ina madhehebu mengi, ambapo suala la madhehebu ni nyeti nchini
humo,hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi
yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea, hiyo ilmsaidia
sana hata kuweza kutoa kitabu kiitwacho ‘Al-Fiqh a’laa madhaahibilkhamsah’
(Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi,
Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka hivi karibuni Inshaallah).
Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya kiswahili
ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya
ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri
wengine.
Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi,
visa vizuri,na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji
atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi
amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasayansi
kama kina Enstein, Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na
wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.
Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka
mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.
Ruhusa imetolewa kwa yeyote anaetaka kukichapisha upya kitabu hiki
kwa sharti tu kwamba asibadilishe chochote bila ya kutujulisha, na
atutumie nakala moja baada ya kukichapisha.
Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa
bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.

 • Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania