Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. ASILI YA USHIA NA MISINGI YAKE (ASLU’SH-SHIA WA USULUHA)

ASILI YA USHIA NA MISINGI YAKE (ASLU’SH-SHIA WA USULUHA)

 • ALLAMAH MUHAMMAD HUSEIN AALE KASHIFUL_GHITA
 • 5000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Katika uandishi uliojaa utata, mara nyingi hudaiwa kwamba
Madhehebu ya Sunni ni “Imani Sahihi” ya Kiislamu na kwamba
madhehebu ya Shia ni “Madhehebu iliyozushwa”, na ni madhehebu
iliyoanzishwa kwa lengo la kufanya mapinduzi ndani ya Uislamu.
Wazo hili wakati mwingine huelezwa kwamba “Ushia” ulianza kama
harakati za kisiasa na baadaye kupata nguvu ya kidini.
Huu upinzani dhidi ya Ushia, haukomi tu kwa Waandishi wa
karne zilizopita, bali hata Wanazuoni wa Kisunni wa karne hii
wanakubaliana na mawazo haya. Wanazuoni kama Abul Hassan Ali
Nadwi, Manzur Ahmad Nu’mani (wote wawili wa India), Ihsa’n Illahi
Zahir (wa Pakistan), Muhibbu ‘d-Din al-Khatib na Mussa Ja’r Allah
(wa Mashariki ya Kati); wanaunga mkono mawazo haya. Nadharia
hii inakubaliwa pia na kikundi cha Wanazuoni waliohitimu kutoka
Seminari za Kidini na ambao hawakusoma kabisa Elimu Dunia.
Fazlur Rahman (wa Pakistan) na Ahmad Amin (wa Misri) wamo
katika kundi hili.
Kitabu Aslu’sh-Shia wa Usuluhakiliandikwa ili kujibu maandishi
ya Ahmad Amin aliyoyaandika katika kitabu chake Fajru’l-Islam.
Mwandishi mashuhuri wa kitabu Aslu’sh-Shia wa Usuluhani
al-‘Allamah ash-Sheikh Muhammad al-Husayn Al-e Kashiful-Ghita
(alifariki 1373 A.H.) ambaye alikuwa mmoja wa Mujtahid mashuhuri
wa karne iliyopita, kwa mukhtasari ameelezea Imani na matendo
ya ibada ya madhehebu ya Shia na halikadhalika michango ya Shia
(miongoni mwa masahaba na tabi’in) katika nyanja mbali mbali za
Sayansi ya Dini katika Uislamu. Katika kitabu hiki amejadili pia mada
kama vile raj’at, ‘Abdulla’h bin Saba’, bada’a,na taqiya.
Tafsiri ya kwanza ya Kiswahili ya Aslu’sh-Shia wa Usuluhailitafsiriwa
na Sheikh Muhammad Nasser (aliyeukubali Ushia hivi karibuni)
katika mwaka wa sitini na nane. Marehemu baba yangu Allamah
2
Sayyid Saeed Akhtar Rizvi alipelekea Mswa’da wa Tafsiri hiyo kwa
Bw. Ibrahim Qassim wa Zanzibar na Agha Sayyid Muhammad Mahdi
Shushtari kwa ajili ya kuhaririwa. Wote wawili kwa pamoja walihariri
nusu ya Mswa’da huu, na nusu iliyobakia ilihaririwa baadaye na Agha
Sayyid Mahdi. Marehemu Agha Mahdi alipohamia Tehran, alianza
kutafsiri upya Aslu’sh-Shia wa Usuluhana ilichapishwa kwa mtiririko
katika matoleo ya Gazeti la Sauti ya Ummachini ya jina “Asili ya
Shi’a” iliyotafsiriwa na Agha Mahdi. Hata hivyo, hiyo haikuwa tafsiri
ya kitabu kamili.
Marehemu baba yangu Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
alipotembelea Iran mwaka 2000, kwa ajili ya matibabu ya moyo,
katika kikao chake na Ayatullah Sayyid Ali al-Khamenai, Kiongozi
huyu mtukufu alionyesha shauku yake ya kuona kitabu Aslu’sh-Shia
wa Usuluhakatika lugha ya Kiswahili.
Baada ya kuipitia sehemu ya tafsiri iliyokuwa tayari wakati huo,
Marehemu Baba alimwambia Sheikh Musabbah Shaban kufasiri
upya kwa lugha ya Kiswahili kutoka kwenye toleo la lugha ya Kiarabu
kilichochapishwa na “Imam Ali Foundation (Qum)”, yenye rejea
fasaha kilichoandikwa na Bw. Alla Al-e-Ja’far, mwaka 1415 A. H.
Unayoiona mikononi mwako ni ile tafsiri mpya.
Tunamuomba Allah (s.w.t.) ateremshe Rehema Zake juu ya Roho
za Mwandishi, Wafasiri wa mwanzo na Wahariri wote. Pia
tunamuomba Allah (s.w.t.) amlipe Sheikh Musabbah kwa kazi hii
na amzidishie Tawfeeq aweze kutangaza na kueneza mafundisho
ya Uislamu wa kweli miongoni mwa Jamii zizungumzao lugha ya
Kiswahili.
Muharram 1426 / Machi 2005   Sayyid Muhammad Rizvi
Toronto, Canada.

 • ALLAMAH MUHAMMAD HUSEIN AALE KASHIFUL_GHITA
 • 5000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 2005