Kiislamu vyanzo

  1. home

  2. book

  3. BARUA YA WAZI KWA MAWAHABI

BARUA YA WAZI KWA MAWAHABI

BARUA  YA WAZI  KWA  MAWAHABI

  • ABDILAHI NASSIR
download

    Download

Rate this post
description book specs comment

Mwanzo mwanzo wa mwezi huu (Muharram 1424), hapa Mombasa, pametolewa karatasi zenye
kichwa cha habari “Barua ya wazi kwa wahubiri na ma-imamu wa sunna”. Lengo la karatasi hizo
ni kuwaonyesha hao wahubiri na maimamu wa kisunni makosa wanayoyafanya ya kuweka “vikao
vya mawaidha, khususan katika siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Muharram”. Kwa maoni ya
waandishi wa karatasi hizo, “hakuna hadith (dalili) ambayo inatuambia tufanye hivyo” isipokuwa
huo ni “uzushi” ambao, kwa kuufanya, “mwawapoteza wafuasi wa Sunna kwa kuwaiga hao hao
Ma-Shia”.
Waliozitoa karatasi hizo wamejiita “Ahlul-Tawheed” ambao, kama wasomi wote wanavyojua, ni
mawahabi. Wao hutumia jina hilo kwa sababu mbili. Sababu ya kwanza ni kuficha uwahabi wao
wanaojua kwamba unapingwa na Waislamu wote. Kwa hivyo wanaogopa kukosa kuungwa mkono.
Sababu  ya  pili  ni  kutokana  na  ile  imani  yao  kwamba  wao  peke  yao  ndio  wanaompwekesha
Mwenyezi Mungu;  Waislamu wengine wote wasiokubaliana nao,  kivyao, ni mushrikina. Lakini
kwa kuwa Waislamu wote wanaamini kwamba ni ahlut tawhiid, kwa vile wote wanaikiri Laa ilaaha
illallaah,  waandishi  wa  karatasi  hizo,  kwa  kutumia  jina  hilo,  wanataka  kuwavungavunga
Waislamu wawafikirie kuwa ni wenzao.
Katika karatasi zangu hizi si nia yangu kuwajibia ndugu zangu, wahubiri na maimamu wa kisunni,
kwa  sababu ninaamini kwamba wao wenyewe wanao uwezo wa kufanya hivyo  –  lau wataona ni
dharura. Nia yangu khaswa ni kujibu yale waliyoyaandika kuhusu mashia na ushia.
1. Katika karatasi zao wamesema: “Waandishi wa ki-Sabai wa Iraq walizua hadithi za urongo, za
kikatili  na  za  kutisha,  kama  vile  kunyimwa  maji  ya  kunywa  (Hussein  na  watu  wake)  na
kulazimishwa kupigana, kukatwa vichwa. Ambazo haziaminiki wala haziwezi kutegemewa na pia
ziko mbali na ukweli.”
Majibu yetu: Penye vitabu vya Kiswahili, viwezavyo kupatikana madukani humu humu mwetu,
hapana haja ya kutaja vitabu vya lugha nyengine ambavyo wengi wa watu hawana au hawawezi
kuvipata  au  hawaijui  lugha  iliyoandikiwa  vitabu  hivyo.  Kwa  hivyo  tuangalie  kitabu  kiitwacho
Maisha ya Sayyidna Huseyn (chapa ya 1999) kilichoandikwa na Sheikh Abdalla Saleh Farsy na
kuchapishwa na Adam Traders wa Mombasa.
Katika uk . 37 wa kitabu hicho, Sheikh Abdalla ameandika hivi: “Alipowajibu  kwa yakini (yaani
Imam Husein) kuwa hakubali kwenda kuuawa na Ubeydillah na kudhalilishwa, wala kuuawa watu
wake na kudhalilishwa, wanaume na wanawake na watoto, waliwazunguka darmadar wasiwe na
njia ya kupenya na kukimbia. Wakakosa maji na chakula tangu hapo mwezi nane Mfunguo Nne
61 mpaka mwezi kumi 61; hapo wakaingia kuwapiga baada ya kuwa hawajifai kwa njaa na kiu”.
Baada ya hayo, akataja orodha ya watu kumi na moja ambao ndio “wa mwanzo kuuawa”; wote
wakiwa ni jamaa zake Mtume (s.a.w.w.)!
Na katika uk . 39 wa kitabu hicho hicho, akasema kwamba baada ya kuuliwa hivyo, walipelekwa
“kwa shangwe kubwa na ngoma mpaka Al Kufa kwa Liwali. Kila mtu akajitapa mbele ya huyo
Liwali ‘Mimi nimemuua fulani …. Mimi nimemuua fulani…’ na huku wanapewa tuzwa (tunza)”.
Wakifika huko, Sheikh Abdalla anasema, ikawa “vichwa vimetawanywa chini”.
Jee, vichwa hivyo vilitoka vyenyewe miilini mwao au vilikatwa?
2.    Wakasema tena katika hiyo karatasi yao: “Na madai ya Mashia kwamba Hussein alikatwa
kichwa chake ni urongo mtupu.”
Majibu yetu: ni tumsome tena Sheikh Abdalla Saleh Farsy. Katika uk . 38 wa hicho kitabu chake,
shekhe  wetu  huyo  anaeleza  kwamba,  baada  ya  kumzingira  “kila  upande  kwa  kumpiga  kwa
mishare, mikuki na panga mpaka akaanguka chini wakamkata kichwa. Na qawli  mashuhuri (ni)
kuwa aliyemkata kichwa ni Shimr bin Dhiljawshan…” Kisha akaongeza: “Pesa na kutaka ukubwa
kunafanya kazi.”
Wala madhalimu hao hawakutosheka tu na kukikata kichwa cha Imam Hussein (a.s). Anavyoeleza
Sheikh  Abdalla  Saleh  Farsy  (uk.  39)  ni  kwamba,  kilipofika  kwa  Liwali  Ubeydillah,  ikawa
“anakigonga  kichwa  cha  Al  Huseyn  kwa  kifimbo  mkononi  kama  kwamba  anapiga  upatu  au
chapuo.” Na kilipofika kwa Mfalme mwenyewe (Yazid bin Muawiya), Sheikh Abdalla anaeleza (uk.
40),  alifanya  “kama  yale  aliyoyafanya  Liwali  wake  wa  Al  Kufa.  Akakamata  kifimbo  akawa
anayagonga meno ya Huseyn …”
Basi hayo ndiyo aliyoyaandika Sheikh Abdalla Saleh Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kenya na,
kabla ya hapo, Zanzibar. Jee, yeye alikuwa “mwandishi wa ki-Sabai wa Iraq ?” Alikuwa Shia? Ni
“mrongo”?  Hakuwa  shekhe  mkubwa  waliyekuwa  wakijifakhiri  naye  hao  “Ahlul  Tawheed”,  na
mpaka leo hujifakhiri naye? Sasa wanasemaje?

  • ABDILAHI NASSIR