Kiislamu vyanzo

  1. home

  2. book

  3. BWANA ABU TALIB [A]

BWANA ABU TALIB [A]

  • Amiraly M.H. Datoo
Rate this post
description book specs comment

MANENO MACHACHE
Bismilahir Rahmanir Rahiim
Alhamdu li waliyyihi was-Salaatu-ala Nabiyyihi wa Aalihil Aimmati wa Awliyail Ummah.
Kitabu hiki kiitwacho Bwana Abu Tallb [a] madhulumu wa historia ni tarjuma ya juzuu ya 7 na 8
ya kitabu mashuhuri kiitwacho AI-Ghadiir cha Allamah al-Amini na ambacho kinazungumzia  hali
ya maisha ya Bwana Abu Talib [a] ambaye ni baba mzazi wa Amir al-Mu’miniin Imam Ali ibn Abi
Talib [a]. Kama vile zilivyofanywa kazi zigine za utafiti basi mtunzi wa kitabu hiki cha Al-Ghadiir
ametimiza wajibu wake pia.
Katika lugha nyingi sana kumeandikwa kwa uchache sana kuhusu Bwana Abu Talib [a] na hayo
machache yaliyoandikwa kuna mambo mengi mno yenye kutatanisha ndani yake. Mazungumzo
makubwa sana katika maisha yake ni kule kuangalia na kutafakari Bwana Abu Talib [a] amefanya
mambo gani na ameyafanyaje mambo hayo katika umri wake huo kwa mujibu wa ushahidi wa
kihistoria ambayo machache yake yamo katika kitabu hiki-tunaona kuwa Bwana Abu Talib [a]
wakati wake mwingi ameutumikia Uislamu na vile vile katika kumhifadhi na kumnusuru Mtume
[s]. Katika hali hii yeye ameweza kuvumilia hasira na ukali wa chuki za kabila lake la Maquraish
kiasi cha yeye na hao wachache walipokuwa wametolewa nje ya mji wakakaa katika Shayb-i-Abu
Talib na wakastahimili matatizo na dhiki zote na wakaweza kufanya subira ya hali  ya juu. Kwa
hakika ni kwamba wakati huo ndio uliokuwa wa harakati na mikakati mipya ya mapinduzi ya
Kiislam ambayo yalikuwa yakitekelezwa na Mtume [s]. Kwa hakika Shayb-i-Abu Talib kisa chake
hicho kinaonyesha wazi uhalifu uliokuwa ukifanywa na Maquraish kisiasa kiuchumi na kimaisha
na kijamii vilevile cihidi ya Mtume [s] na watu wake. Katika hali ngumu kabisa kama hizi na
zinginezo tulizonazo katika historia Bwana Abu Talib kwa nyakati mbalimbali ameweza kujitolea
yeye mwenyewe kumnusuru na kumlinda Mtume  [s] na vile vile amewaamrisha wanawe Ali [a]
na Jaafer [a] wawe daima wakijitolea kwa ajili ya kumnusuru na kumwokoa Mtume [s]. Kwa
mukhtasari kabisa tunaona kuwa maisha yake yote alikuwa ameshajitolea katika kuunusuru na
kueneza  Uislamu  na  kumwokoa  na  kumkinga  Mtume  [s]  kwa  sababu  tu  yeye  alikuwa
amekwishaongoka na kupata hidaya ya Islam. Yeye wakati wa mwisho wa pumzi yake alikuwa
akiwasisitiza  na  kuwahimiza  watoto  na  jamaa  zake  wawe  daima  mbele  katika  kumnusuru  na
kumkinga na kumuunga mkono Mtume Muhammad [s] katika kueneza Uislamu. Na vile vile kwa
kifo  chake  (ambacho  kilikuwa  baada  ya  kifo  cha  Bi  Khadijat-il-Kubra)  Mtume  [s]  alikuwa
amehuzunika mno kiasi kwamba alikuwa ameutangaza mwaka huo kuwa ni aamul huzun yaani
mwaka wa huzuni kubwa.
Kwa kupata mwangaza huo bado tunaona katika vitabu vingine vya kihistoria vya madhehebu
mengine yakiwa yanamtaja Bwana Abu Talib kuwa ni mushrik na kuthubutu kumsema kuwa ni
kafiri.  Kwa  hakika  tuhuma  kama  hizi  katika  historia  ni  njama  kubwa  sana  zilizofanywa  na
wamejaaribu hao waliotoa tuhuma hizo kuthibitisha tuhuma zao kwa aya za Qurani tukufu na
hadithi za Mtume [s].
Kama tutakavyoweza kuona vyema madhumuni makubwa ya hawa watoao tuhuma kwa kusema
Bwana Abu Talib ni mushrik na kafiri huku wakimchukulia yeye kuwa ni mtu mmoja wa kawaida
lakini siri ya malengo yao ni kule kuthibitisha kuwa baba yake Imam Ali ibn Abi Talib [a] alikuwa
ni mushriki na kafiri ili waweze kumvunja nguvu Imam Ali [a]. Ni dhahiri kuwa ni jambo ambalo
tunalielewa kuwa iwapo baba atapata pigo basi shida hiyo kubwa itamfikia na kumwathiri mtoto
wake katika maisha na nyadhifa zake. Lakini kama tulivyokwisha kuona kuwa malengo yao sio
Bwana Abu Talib mwenyewe bali wao wanataka kumdhoofisha na kumvunja nguvu Imam Ali [a]
kuwa baba yake alikuwa hana imani na alikuwa mushriki na kafiri ili kwamba Imam Ali [a] hali
na maisha yake yawe na dosari kubwa.
Vyote  tulivyokwisha  kuvisoma  hapo  juu,  usahihi  wake  au  uwazi  wake  unakuwa  pale  wakati
tunapoona kuwa historia hii hii na waandishi hawa hawa  na wanonakili riwaya hawa hawa ambao
wanatoa uamuzi kama huo kuhusu Abu Talib [a] –  wanakaa kimya kuhusu wazazi wao waliokuwa
wakija daima mbele ya Imam Ali [a] katika maisha yao –  wao daima wamekuwa wakiyeyuka mbele
ya nuru ya Imam Ali [a] kwa kutoweza kustahimili nuru hiyo. Tunaona kuwa waandishi hawa
hawa  na  wanaoripoti  riwaya  hizi  ndio  wanaoandika  fadhila  zake  lakini  tunashangaa  kuona
pamoja  na  kuandika  sifa  na  fadhila  na  daraja  zake  makabila  yao  na  watu  wao  wanashindwa
kupambanua upotofu huu ulivyo ndipo hapo tunaona kuwa Allamah Amin amefanya utafiti wa hali
ya juu usio na kifani na ameweza kuchambua historia kwa undani kabisa pamoja na matukio na
riwaya na ametupatia matunda mazuri mno ya kazi yake ambayo imejibu na imeweza kuondoa
tuhuma zote dhidi ya Bwana Abu Talib [a] kuwa yeye alikuwa ni mushrik na kafiri. Bwana Amini
ameweka uwanja wazi kama tutakavyoweza kushuhudia wenyewe kuwa Bwana Abu Talib kamwe
hakuwa mushrik wala kafiri.
Hata hivyo inabidi  kitabu kijiarifishe chenyewe  hivyo sisi tunayafupisha mazungumzo haya ili
msomaji aweze aweze kujibwaga katika uwanja wa utafiti ili kufikia majibu na kuwapima viongozi
wanaotoa tuhuma dhidi ya Bwana Abu Talib [a].

  • Amiraly M.H. Datoo