Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. FADAK

FADAK

 • ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI
 • 2000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
download

  Download

5 (100%) 1 vote[s]
description book specs comment

DIBAJI
Tunamshukuru Allah (s.w.t.), kwa Baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na
Watukufu Ahlul~Bait (a.s.) kwa kutujaalia kuweza kufanikisha juhudi zetu
hizi katika kuchapisha kitabu hiki “Fadak”.
Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya moja ya maandishi vya
Marhum Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a.). Kitabu hiki kimekuwa
maarufu katika ulimwengu wa Ki-Islamu na kilitafsiriwa na kuchapishwa
na Taasisi mbali mbali kwa lugha ya Ki-Urdu, Ki-Hindi na Ki-Gujrati.
Sababu iliyoifanya Bilal Muslim Mission isimamie kazi hii ni kama ile za
mwanzo, ambayo inatokana na maombi ya watu wengi kutoka Afrika ya
Mashriki kutaka kujua kadhia ya muhimu na ya maana sana katika historia
ya Uislamu, kadhia ya Fadak. Hii ilitufanya tutafsiri na kuchapish kitabu
hiki kwa lugha ya kiswahili ili watu wazungumzao kiswahili wa weze
kuelewa na kufahamu dhuluma na maonevu yaliyotendwa kwa Ahlul Bayt
(a.s.) watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.).
Mimi binafsi sikusita kumuomba ndugu yetu Dr Muhammad Kanju
kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka kwenye asili yake
ya lugha ya Kiingereza, Namshukuru Dr Kanju kwa kukubali ombi langu
na kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja.
Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale wote ambao
kwa juhudi zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi mwao na
wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine katika kazi zetu
za Tabligh.Tunamuomba Allah (s.w.t.) awalipe malipo mema hapa Duniani
na baadaye huko, Akhera.

 • ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI
 • 2000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 2004
 • 1
 • Dar es Salaam, Tanzania