Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. FATIMA Al-ZAHRA

FATIMA Al-ZAHRA

 • Sayyid Muhammad al-Husaini al-Shirazi
 • AL-ITRAH FOUNDATION
 • 2008
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu
kiitwacho, Fatimah al-Zahra.Sisi pia tumekiita, Fatima al-Zahra.
Kijitabu hiki ambacho kimepambwa kwa jina la Fatima Zahra (a.s), binti
wa Mtume Muhammad (s.a.w.), ni kati ya mihadhara ya thamani ya mare-hemu Imam Muhammad al-Husaini al-Shirazi (Mwenyezi Mungu amrehe-mu).
Ni kitabu cha aina yake katika lugha ya Kiswahili kinachoelezea maisha ya
Bibi huyu mtukufu mwenye nuru. Cha kuzingatia ni kwamba kumjua
mtukufu huyu ambaye ni Bibi wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) ni
wajibu kwa Waislamu wote, kwani ameshasema: “Jueni kwamba mimi ni
Fatima al-Zahra.” Yaani kunijua mimi ni wajibu kwa kila muumini. Bibi
Fatima (a.s.) ni maasumu wa pekee katika jinsia yake, kumpenda kwake na
kumtawalisha kwake ni sawa na kumpenda na kumtawalisha Amirul
Muuminina Ali (a.s) na watoto wake walio maasumu (a.s).
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa
maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano
za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena
katika akili za watu.
Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua
kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale
ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 5/25/2009 8:27 AM Page D
Tunamshukuru ndugu yetu, Abdul Karim Juma Nkusui kwa kukubali juku-mu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote
walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa
kwake.

 • Sayyid Muhammad al-Husaini al-Shirazi
 • AL-ITRAH FOUNDATION
 • 2008
 • la kwanza