Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. FITINA ZA WAHHABI ZAFICHULIWA

FITINA ZA WAHHABI ZAFICHULIWA

 • ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI
 • 5000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Tunamshukuru Allah (s.w.t.), kwa Baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)
na Watukufu Ahlul-Bait (a.s.) kwa kutujaalia kuweza kufanikisha
juhudi zetu hizi katika kuchapisha toleo la saba la kitabu hiki “Fitina
Za Wahhabi Zafichuliwa.”
Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya moja ya ma’andishi
ya Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a.). Kitabu hiki
kimekuwa maarufu katika ulimwengu wa Ki-Islamu na kilitafsiriwa
na kuchapishwa na Taasisi mbali mbali kwa lugha ya Ki-Ingereza,
Ki-Urdu na Kiarabu.
Sababu iliyoifanya Bilal Muslim Mission isimamie kazi hii ni kama
zile za mwanzo, ambayo inatokana na maombi ya watu wengi kutoka
Afrika ya Mashriki kututaka tuchapishe Kitabu hiki kwa lugha ya
Kiswahili.
Hii ilitufanya tutafsiri na kuchapish kitabu hiki ili watu wazungumzao
kiswahili waweze kuelewa na kufahamu zaidi juu ya suala hili na fitina
hizi za maadui wa Uislamu.
Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa mfasiri wa
kitabu hiki Ndugu Dr. Mohammad Kanju na wale wote ambao kwa
juhudi zao toleo hili la saba la kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu
mikononi mwao na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au
nyingine katika kazi zetu za Tabligh. Tunamuomba Allah (s.w.t.) awal-ipe malipo mema hapa Duniani na baadaye huko, Akhera.

 • ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI
 • 5000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 2005
 • Toleo ya Saba
 • Dar es Salaam, Tanzania