Kiislamu vyanzo

  1. home

  2. book

  3. GUZO YA UCHAMUNGU Imamu Muhammad Taqi [a]

GUZO YA UCHAMUNGU Imamu Muhammad Taqi [a]

  • Sayyid Ali Naqi Saheb
download

    Download

Rate this post
description book specs comment

Maisha ni nguvu isiyoonekana kwa macho na ambayo haipimiki kwa miaka isipokuwa kwa mkazo wa nguvu ya maendeleo iliyoko ndani yake. Maisha ya namna hii yanapotokea katika hali ya kawaida ya mambo ya ulimwengu yanaacha alama zisizofutika kuliko yale maisha ambayo yangekuwa na urefu wa miaka elfu moja.
Maisha ya Imamu Muhammad Taqi [a] ni mfano wa maisha ya namna hiyo. Ingawa aliishi kwa muda wa miaka michache zaidi kuliko Imamu yeyote yule kati ya Maimamu hao kumi na wawili [a], maisha yake ni muhimu kama yale ya Imamu yeyote yule mwingine kwani alikuwa na tabia sawa na Maimamu wengine, aliutangaza ujumbe ule ule na alikuwa ni Mwali wa Nuru ile ile.

  • Sayyid Ali Naqi Saheb