Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. HADITH ZA MTUME s.a.w.w. NA MA-IMAMU a.s 2.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w. NA MA-IMAMU a.s 2.

HADITH ZA MTUME s.a.w.w.   NA MA-IMAMU a.s 2.

 • BUKOBA - TANZANIA
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Allah swt anatuambia katika Al-Qur’an tukufu: Sura al-Nahl, 16,
Ayah 43
Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi
(Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.
Sura Al-Ambiya, 21, Ayah 7
Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa Wahyi
(ufunuo). Bas waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui.
Ayah  hii  Tukufu  inawasihi  Waumini  kujielekeza  kwa  Ahl-Dhikr  yaani
watu  wenye  busara  na  Wanazuoni  wa  Ummah  ili  kuweza  kubainisha
baina ya haki na batili, wakati ambapo  Waumini wanapokumbana na
shida au ugumu katika masuala mbalimbali, kwa sababu Allah swt baada
ya  kuwafundisha  ilimu,  aliwachagua  hao  kwa  hayo.  Hivyo,  wao
wamebobea  katika  ilimu  na  ambao  ndio  watu  halisi  wanaoielewa,
kuifundisha na kuitekeleza kwa usahihi mafunzo ya Qur’an.
Ayah hii iliteremshwa kwa ajili ya kuwatambulisha Ahlul-Bayt a.s. nao
ni  Mtume  Muhammad  Mustafa  s.a.w.w.,  Al  Imam  ‘Ali  ibn  Abi  Talib
a.s.Fatimah a.s., Al-Imam Hassan ibn Abi Talib a.s. na Al-Imam Husayn
ibn  Al  Imam  ‘Ali  ibn  Abi  Talib  a.s.  ,  ambao  kwa  ujumla  wanaitwa
Watukufu watano au ‘Al-i-‘Aba ambapo pamoja na hao wameongezeka
Ma-Imamu a.s. wengine tisa kutokea kizazi cha al-Imam Husayn ibn Al
Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.mara
nyingi katika nyakati mbalimbali aliwatambulisha hao kuwa ni Ma-Imam
waongozi, nuru katika kiza, na ni wale ambao wamebobea katika  ilimu
na bila shaka Allah swt amewajaalia Ilimu ya Kitabu Kitukufu.
Ukweli huu, kama ilivyorejewa mahala pengi katika Ahadith mbalimbali
kuanzia  zama  za  Mtume  Muhammad  Mustafa  s.a.w.w.kuanzia  ufunuo
hadi  leo  hii,  na  vile  vile  wanazuoni  wengi  na  Wafasiri  kutokea  AhlSunnah wamekiri waziwazi katika vitabu vyao kuwa Ayah hizi za Qur’an
zilikuwa  zimeteremshwa  hususan  kwa  ajili  ya  kuelezea  na
5
kuwatambulisha Ahl-ul-Bayt a.s. Baadhi ya mifano ya vitabu vyenyewe
ni kama ifuatavyo:
1.  Imam Tha’labi katika tafsiri ya kitabu chake juu ya Ayah hiyo ya
42 kutokea Sura An-Nahl, namba 16
2.  Tafsir ibn Kathir, j.2, Uk.591
3.  Tafsir at-Tabari, j.14, Uk.75
4.  Tafsir-i-Alusi, ijukanavyo kama: Rahul-Bayan , j. 14, Uk. 134
5.  Tafsir-i-Qartabi, j.11, Uk. 272
6.  Tafsir-i-Hakim, au Shawahid-ut-Tanzil,  j. 1, Uk. 334
7.  Tafsir-i-Shabistrary, au: Ihqaq-ul-Haq,  j.3, Uk.482
8.  Yanabi’-ul-Muwaddah, cha Ghanduzi Hanafi, Uk. 119
Kwa kutegemea ukweli huu, sisi lazima tujielekeze kwa Wananyumba ya
Ahlul-Bayt  a.s.,  na  kutekeleza  maneno  yatuongozayo  ili  kuelekeza
maisha  yetu  mema.  Kwa  sura  hii,  Imam-ul-Hadi  a.s.  anasema  katika
Man la Yahdhuruh-ul-Faqih, Tahdhib na ‘Uyun-i-Akh-bar-ur-Ridha :
“Maneno  yenu  yenye  busara  yanatupa  nuru,  maamrisho  yenu  ni
hidaya kwa watu na usia zenu ni Taqwa na usawa.”

 • BUKOBA - TANZANIA