Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. HADITHI YA THAQALAINI KATIKA VITABU VYA AHLI SUNNA

HADITHI YA THAQALAINI KATIKA VITABU VYA AHLI SUNNA

 • Dk. Sayyid Alaauddin al-Sayyid Amir Muhammad al-Qazwini
 • 1000
 • Alitrah Foundation
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabu
kiitwacho, Hadith ath-Thaqalaynkilichoandikwa na Dk. Sayyid Alaauddin
al-Sayyid Amir Muhammad al-Qazwini. Sisi tumekiita, Hadithi ya
Thaqalain.
Kitabu hiki, Hadith ya Thaqalainni hadithi maarufu sana katika ulimwen-gu wa Kiislamu. Hakuna madhehebu ya Kiislamu hata moja ambayo
haikutaja hadithi hii, ingawa kuna tofauti kidogo ya mapokezi kati ya
wasimulizi wake. Pamoja na hayo, ukweli unabakia palepale kwamba
haitakamilika historia ya Uislamu bila ya kuitaja hadithi hii. Hadithi ya
Thaqalain ni wasia ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.) alioutoa kwa Waislamu
pale Ghadir Khum wakati anarudi kutoka kwenye Hija yake ya mwisho
(maarufu kama Hijjatu ’l-Widaa). Qur’ani inatuthibitishia kwamba
Uislamu ulikamilika baada ya tukio hili la Ghadir Khum ambapo Mtukufu
Mtume (s.a.w.) alitoa khutba ndefu ambayo kwayo alitoa kauli hii inayo-julikana kama hadithi ya Thaqalain: “…Ninakuachieni vizito viwili
(thaqalayn);Qur’ani Tukufu na Kizazi changu…” Baada ya tukio hili la
Ghadir, aya ifuatayo iliteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.): “…Leo
nimekukamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema Yangu, na nime-wapendeleeni Uislamu uwe dini yenu…”(5:3)
Baada ya kushuka aya hii, Mtukufu Mtume (s.a.w.) alimwita Ali juu ya
mimbari ambayo ilitengenezwa kwa matandiko ya ngamia, kisha akanyun-yua mkono wake akasema: “Man kuntu mawlahu fahadha Aliyyun
mawlahu.”(Yule ambaye mimi ni mwenye kutawalia mambo yake basi
huyu Ali (naye) ni mwenye kutawalia mambo yake.” Kisha akaomba dua:

“Ewe Allah! Msaidie mwenye kumsaidia (Ali) na mpige vita mwenye
kumpiga vita (Ali).” (Rejea ya hadithi hii utaipata kwenye kitabu hiki
kadiri unavyoendelea kusoma)
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa
maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano
za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena
katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah
Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili
kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan
wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini
na ya kijamii.
Tunamshukuru ndugu yetu, Ustadh Amir Musa kwa kukubali jukumu hili
la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki
kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

 • Dk. Sayyid Alaauddin al-Sayyid Amir Muhammad al-Qazwini
 • 1000
 • Alitrah Foundation
 • Januari, 2009
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania