Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. HAJA YA DINI

HAJA YA DINI

 • Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 1999
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu hiki ni tafsiri ya kitabu chake kiitwacho Need of Religion
alichokiandika kwa lugha ya Kiingereza, kwa ajili ya vijana
wa Kiislamu wanaochukua Stashaada (Diploma) ya Elimu ya
Kiislamu kwa Njia ya Posta.
Nimeona kuwa kitabu hiki kitawasaidia sana ndugu zangu
Waislamu wa hapa Afrika ya Mashariki, iwapo nitakitarajumu
kwa Lugha ya Kiswahili, lugha ambayo hutumiwa sana hapa
kwetu.
Kila mtu hupenda kitu na kukithamini sana baada ya kukiona
kuwa ni cha faida kake. Kadiri ya faida ya kitu hicho itakavyozidi
ndio jinsi mtu huyo atakavyozidi kukithamini na kukipenda kitu
hicho.
Dini nayo ni hivyo hivyo. Mtu ataipenda tu, baada ya kuzielewa
faida zake kwake.
Katika kijitabu hiki, ndugu yetu Maulana Sayyid Saeed Akhtar
Rizvi, kwanza anaeleza Dini ni nini, kisha anaelezea faida zake,
anakanusha hoja za wale wasemao kuwa dini ni kitu kipingacho
2
sayansi n.k. Analinganisha dini na “Maendeleo na Mabadiliko
ya viumbe”, halafu anakanusha hoja za wale wasioamini kuwepo
kwa siku ya Ufufuo. Mwisho kabisa anamalizia kwa kuzitaja sifa
muhimu za dini.
Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu aliyemjaalia ndugu yetu
Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi kwa elimu na akatunufaisha
sisi Waislamu wa hapa Afrika Mashariki na duniani pote kwayo.

 • Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 1999
 • Toleo ya Tano