Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. HAKI ZAWANAWAKE KATIKA UISLAMU

HAKI ZAWANAWAKE KATIKA UISLAMU

HAKI ZAWANAWAKE KATIKA UISLAMU

 • Allamah Murtaza Mutahhari
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza,
kwa jina la: “Woman and her rights.” Sisi tumekiita: “Haki za wanawake
katika Uislamu.”
Kitabu hiki, “Haki za wanawake katika Uislamu” ni matokea ya utafiti
wa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu, Allamah
Murtaza Mutahhari.
Allamah Murtaza Mutahhari, mwandishi wa kitabu hiki ameichambua historia
ya maisha ya mwanamke katika nchi za Magharibi na Mashariki
(Asia) na mifumo yao ya ndoa. Mwandishi amerejea vyanzo vya wanasaikolojia
na wanasosholojia wa Magharibi ili kuthibitisha hoja zake.
Madhumuni yake ni kutaka kuthibitisha kwamba Uislamu una mfumo
mzuri wa ndoa na haki za wanawake, kinyume na wanavyoamini watu wa
Magharibi na wengine waliokuwa na kasumba ya umagharibi.
Inakubaliwa na kila rafiki na adui kuwa Qur’ani Tukufu ilifufua haki za
wanawake. Hata maadui wanakiri angalau kwamba Qur’ani wakati wa
kuteremshwa kwake ilichukuwa hatua kubwa katika kuboresha hali ya
mwanamke na kurejesha haki zake za binadamu. Qur’ani ilifufua haki za
mwanamke kama mwanadamu na kama mwenzi wa mwanaume katika utu
na haki za binadamu lakini haikupuuza jinsia yake wala jinsia ya
mwanaume. Kwa maneno mengine Qur’ani haikupuuza maumbile ya
mwanamke. Ndio maana kuna kuwafikiana kikamilifu kati ya kanuni za
maumbile na kanuni za Qur’ani. Mwanamke katika Qur’ani ni sawa na
mwanaume katika maumbile. Vitabu hivi viwili vikubwa vya kimungu
(Qur’ani na maumbile), kimoja kikiwa kimeumbwa na kingine kikiwa
kimekusanywa, vinakubaliana na kuafikiana kabisa. Nia ya kitabu hiki nikuangazia na kuelezea kuafikiana huku.
Kutokana na umuhimu wa maudhui hii tumeona tukitoe kitabu hiki kwa
lugha ya Kiswahili ili kutoa mwanga kwa Waislamu wazungumzaji wa
Kiswahili.
Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo
makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi
yetu ya ‘Al-Itrah Foundation’ imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya
Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu,
hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala
ya dini na ya kijamii.
Tunamshukuru ndugu yetu, Aziz Njozi kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia
tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki
kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

 • Allamah Murtaza Mutahhari
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania