Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. HIJAB VAZI LA MWANAMKE WA KIISLAMU

HIJAB VAZI LA MWANAMKE WA KIISLAMU

HIJAB VAZI LA MWANAMKE WA KIISLAMU

 • Muhammad Ibrahim Kadhim Al-Qaz-wini.
 • Toleo la Pili
 • Dar-es-Salaam, Tanzania
download

  Download

2.8 (55%) 4 vote[s]
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha
Kiarabu, kwa jina la: Al-Hijab Saa’datun laa shiqaaun, kilichoandikwa
na, Sheikh Muhammad Ibrahim El-Qazwiniy
Kitabu hiki kinahusu vazi la Hijabu; vazi ambalo ni rasimi kwa
wanawake wa ki-Islamu kwa ajili ya kustiri maungo yao. Maadui
wa Uislamu wanalibeza sana vazi hili kiasi cha kutaka
kuwakatisha tamaa wavaaji wake – ambao ni wanawake wa ki-
Islamu. Mazingira ya sasa tayari yanaonesha kwamba, azma ya
maadui hawa wa Uislamu kiasi fulani inafanikiwa. Kwani sasa hivi
katika miji yetu asili mia kubwa ya wanawake wanatembea nusu
uchi, na hali ni mbaya sana. Hivyo tulipo kiona kitabu hiki,
tukaona ni wakati muafaka tukitoe kwa lugha ya kiswahili, kwa
kutekeleza amri ile ya Mwenyezi Mungu ya, “kuamrisha mema na
kukataza maovu.”
Mwandishi wa kitabu hiki ameelezea kwa ufasaha sana falsafa na
hekima ya vazi hili, na kuvunja hoja za wale wote wanaolipinga.
Katika kufanya hivyo ametumia elimu, akili na hoja zenye mantiki.
Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Msabah S. Mapinda kwa
kukubali kwake kuchukuwa jukumu hili la kutarjum kitabu hiki,
kutoka lugha yake ya asili ya Kiarabu kwenda lugha ya Kiswahili.
Halikadhalika tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia
moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.
Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa
kwa wasomaji wetu, hususan wanawake wa ki-Islamu na
kuiokoa jamii yetu kutokana na maovu.

 • Muhammad Ibrahim Kadhim Al-Qaz-wini.
 • Toleo la Pili
 • Dar-es-Salaam, Tanzania