Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. HISTORIA YA CHANZO CHA MAWAHHABI

HISTORIA YA CHANZO CHA MAWAHHABI

 • Sharrif Sagaf Ahmed
 • 1000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kuanzia mazungumzo yangu, natanguliza aya ifuatayo
kama dibaji ya maudhui yenyewe. Mwenyezi Mungu
Mwenye Rehma amesema katika Qur’ani tukufu kuwa:
“Akasema: Hakika wafalme wanapouingia mji,
wanauharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa
dhalili; hivyo ndivyo wanavyofanya”. (27:34)
Aya hii inatoa ujumbe kwa Waislamu ulio muhimu
sana. Inaeleza kwamba unapotokea ufalme usiotosheka
na milki yake na ukawa na nia ya kutaka kupanua
himaya yake na mipaka yake, basi daima ufalme
kama huu hauwezi kuzingatia kanuni za haki katika
nidhamu yake. Na hapo ufalme huo hupotoka na
kuanza kuvamia nchi nyingine na kuiteka miji yake
na kufanya ufisadi ikiwa ni pamoja na kuharibu mali
na kuhilikisha maisha ya wanadamu. Kwa kuwa
Mawahhabi historia yao inaonyesha kutokana kwao
na mambo ya ufalme na mauaji hapana shaka kuwa
aya hii inazungumzika katika fitna yao.

 • Sharrif Sagaf Ahmed
 • 1000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 2003
 • Toleo ya Sita
 • Dar es Salaam, Tanzania