Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. HUKUMU ZA KIFIKIHI ZINAZOWAHUSU WANAWAKE

HUKUMU ZA KIFIKIHI ZINAZOWAHUSU WANAWAKE

 • Mustafa Ranjbar Shirazi
 • 10000
 • Toleo la kwanza
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu
kiitwacho, Fiqhu ‘l-Fatayaat kilichoandikwa na Mustafa Ranjbar wa
Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran .
Kitabu hiki chenye manufaa sana kinahudumia mahitaji ya wajibu wa dini
ya Kiislamu ya mwanamke kuhusiana na vipindi vyake vya kila mwezi.
Baadhi ya mas’ala na hukumu za kuhudumia maiti ni makala muhimu zilizoongezwa
kwenye kitabu hiki.
Sharia na kanuni zilizowekwa na Uislamu kwa ajili ya namna ya maisha ya
usafi iliyodhibitiwa ni wajibu kwa kila Mwislamu kujifunza na kuzipandikiza
ndani ya nafsi yake. Hili ni dhahiri kabisa kwamba litamwezesha
yeye kudumu ndani ya mipaka ya mahitaji ya kisharia yaliyowekwa.
Shukrani zetu nyingi zimwendee ndugu yetu Ukhti Maysara Ali kwa kazi
yake ya kutarjumi kitabu hiki. Vilevile shukrani zetu kwa wale wote
waliochangia kwa njia moja au nyingine kwenye kufanikisha kukamilika
kwa kazi hii tukufu.

 • Mustafa Ranjbar Shirazi
 • 10000
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania