Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Sunna

 • Sheikh Jafar Subhani
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha
Kiarabu kwa jina la: “Al-Qabdh Baina ‘l-Bid’ah wa ‘s-
Sunnah” Sisi tumekiita: “Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au
Sunna? Kwenye Sala.”
Kitabu hiki, “Je, Kufunga Mikono Ni Bidaa au Sunna? Kwenye
Sala” ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na
Mwanachuoni wa Kiislamu, Jafar Subhany.
Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila
jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata
mwanadamu katika sekta zote za maisha yake.
Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu wamehitilafiana
katika hukumu ndogo ndogo katika matendo ya
ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanachuo kwa
wafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zongo
lisilo na maana. Mambo ambayo wanachuo wetu wamehitilafiana
si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo
machache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo.
Kufunga mikono kwenye Sala ni suala ambalo wanachuo wetu
wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya
wanachuo wa madhehebu zote wamehitilafiana juu ya suala
hili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitilafu
hii kwa usahihi na hivyo kuongelea katika dhana na kusababisha
mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii
Sheikh wetu, Jafar Subhani amelifanyia utafiti wa kina suala
hili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachia
msomaji mwenyewe kutoa uamuzi.
Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa
maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na
ukweli huu, Taasisi yetu ya ‘Al-Itrah Foundation’ imeona ikitoe
kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale
yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa
Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya
kijamii.
Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani
(Lipumba) kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma
kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki
kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa
kitabu hiki.

 • Sheikh Jafar Subhani
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania