Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. KUANZIA NDOA HADI KUWAWAZAZI

KUANZIA NDOA HADI KUWAWAZAZI

KUANZIA NDOA HADI KUWAWAZAZI

 • Abbas na Shaheen Merali
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza
kiitwacho From Marriage to Parenthood. Sisi tumekiita, Kuanzia Ndoa
Hadi Kuwa Wazazi.
Kitabu hiki kinazungumzia masuala yote yanayohusu wanandoa: kuanzia
kufunga kwao ndoa – waishi vipi, mpaka watakapopata watoto – wawalee
vipi – kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Kama ambavyo inafahamika
kwamba Uislamu ni dini na ni mfumo wa maisha, basi kwa hakika
haukuacha hata kitu kimoja kinachohusu maisha ya mwanadamu,
pamoja na kumhudumia kiroho.
Ndoa ni taasisi ambayo iliasisiwa na Allah ‘Azza wa Jallah Mwenyewe
pale alipowaunganisha baba yetu Adam na mama yetu Hawa kuishi pamoja
kama mume na mke.
Kwa hiyo, Uislamu kama dini na mfumo wa maisha, umeweka kanuni,
sheria na hukumu za kufuatwa ndani ya taasisi hii tukufu (ya ndoa).
Waandishi wa kitabu hiki wamefanya juhudi kubwa ya kukusanya
mafundisho yote muhimu yenye kuhusu taasisi hii kutoka katika vyanzo
vikubwa na chimbuko la sheria na mafundisho ya Uislamu, ambavyo ni
Qur’ani na Sunna
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa
maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli
huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki
kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia
Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru ndugu yetu, Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali
kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki
kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

 • Abbas na Shaheen Merali
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania