Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. Kuhuzunika n na K Kuomboleza Harakati za Bibi Zainab

Kuhuzunika n na K Kuomboleza Harakati za Bibi Zainab

 • Sayyid Jawad Naqvi
 • 1000
 • AL-ITRAH FOUNDATION
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni kazi nyingine nzuri ya Ustadh
Seyyid Jawad Naqavi. Tukio la Karbala na Ashura ambalo ni bahari
yenye lulu zake zilizowekwa ndani kwenye kina, zinaweza tu kugunduli-wa na wale ambao wamelainishwa kabisa kwa fikra za Imamu Khomein
(r.a) na kufanya mapinduzi ya marekebisho ya moyo wa kijamii katika
jamii ambayo imeathiriwa na maradhi ya kijamii na ya vikundi mbali mbali
vya kijamii. Huu ulikuwa ujumbe wa Imamu Husein (a.s), njia ya Kiongozi
wa Mashahidi (wahanga) na hali halisi ya safari ya mateka kutoka Karbala
kwenda mji wa Kufa, na kutoka Kufa mpaka Syria. Safari hii ya shujaa
dada yake Husein Ibn Ali (a.s) aliibadilisha kuwa harakati ambayo
ilionekana kama iliyolengwa kubadilishwa kuwa kama safari ya mateka
masikini, wanyonge na wachovu. Hutuba za Bibi Zainab (as) zilizopakwa
rangi ya damu ya Husein na masahaba zake watukufu iliutikisa umma na
ufalme wa Yazid. Ilikuwa ni juhudi za watoto wa Fatima na Ali (as) –
Husein na Zainab (as) – ambazo zimeifanya Karbala kuwa Hamasa ya
kudumu na kuvunja majaribio yote katika zama tofauti ya kubadilisha
tukio hili kuwa ugomvi wa kifamilia au tukio linalofaa tu kufanyiwa kum-bukumbu, kupatisha thawabu na kafara la dhambi.
Kitabu hiki ni tarjuma ya makala tatu zilizoandikwa na Ustadh Syed
Jawad Naqvi katika jarida lake linalotoka kila baada ya miezi miwili; bi-monthly magazine Mashrabe Naabla mwezi wa Muharram – Safar.
Vilevile kitabu hiki kina sura ya mwisho ambayo ni moja ya tarjuma ya
hutuba nyingine. Sura zote nne katika kitabu hiki zimelenga katika
kumuamsha msomaji na kufanya maumivu katika moyo wake kuelekea
kwenye mateso katika zama yake ambayo ni kioo cha taswira ya kile ambacho kilitokea wakati wa Imamu Husein (a.s). Chini ya mwanga wa
hatua za Imam Husein, maneno na tabia yake, kitabu hiki humshawishi
msomaji kwamba wakati hali inayokuzunguka ni sawa na ilivyokuwa
wakati wa Husein Ibn Ali (as) na Zainab bint Ali (as), basi na wewe vilevile
unahitaji kuonesha tabia kama ile ile iliyooneshwa na watu wa Karbala.
Hakuna uhalali au sababu yoyote ambayo itakubaliwa kwa ajili ya kukaa
kimya bila kufanya chochote wakati watawala madhalimu wanatawala
jamii, wakati maziwa na mito ya maji inapobadilika kwa damu za watu
wasio na hatia.
Sura ya kwanza ya kitabu hiki ambayo ni mada ya kitabu hiki huelezea na
kufichua asili halisi ya Azadari ambayo ni harakati ya haki kuelekea
kwenye kuiangamiza dhulma na ukandamizaji. Katika sura ya pili, ambayo
imepewa jina la “Ujumbe wa Ashura” ambao kama haukueleweka
unakuwa chanzo cha msingi cha kudorora na ukosefu wa harakati. Sura ya
tatu juu ya “Hamasa-e-Husein” huwasilisha jina halisi la somo la tukio la
Karbala ambalo limekuwa lenye kuathiriwa na upotofu na limegeuka kuwa
kitu kingine mbali na kitu kinachohusika na harakati. Sura ya nne ina
habari kama zile zile za sura ya tatu lakini pamoja na uchambuzi wa kihis-toria na mazingira ambayo yaliwafanya watu wapoteze matumaini na
kuwa chini ya shinikizo lenye matokeo ya ukimya.
Kitabu hiki ni johari nyingine na ni kazi ambayo haiishii kwa Mashia tu,
bali ni kitabu cha Ummawote wa Kiislamu, na kwa kweli kwa wale
wanadamu wote ambao wana maadili fulani yaliyo hai ndani yao.
Namshukuru sana Allah (s.w.t) mara nyingine tena kwa kunibariki kwa
fursa hii kubwa kuwa njia ya kufikisha ujumbe huu wa haki, wenye
kuamsha harakati kwa jumuiya ya wazungumzaji wa Kiingereza (na sasa
kwenye jumuiya ya wazungumzaji wa Kiswahili).
“Ewe Allah! Wakati wowote kama kuna haja ya huduma
kwenye dini Yako, nipe kipaumbele na nifanye mimi wa
mbele zaidi kama njia ya kufikisha.” Imam Sajjad (a.s).

 • Sayyid Jawad Naqvi
 • 1000
 • AL-ITRAH FOUNDATION
 • Octoba, 2010
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania