Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. KWA NINI MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) ALIOA WAKE WENGI?

KWA NINI MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) ALIOA WAKE WENGI?

 • Jumuiya ya Dar-Rahe-Haq Qum, Iran
 • 2000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Mwanzoni mwa karne ya kumi na nane waandishi wa Kikristo
waligundua mbinu mpya za kuushambulia Uislamu. Nia yao ilikuwa
ni kuyaeneza maandishi yasiyo na ukweli ili kupotosha watu kutoka
katika lengo na msingi mathubuti wa Kiislamu na kuitweza heshima
ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w.).
Kiini cha uzushi huo kilikuwa ni vitabu vilivyoandikwa na
waandishi wa Kikristo wa karne ya kumi na tano. Mwandishi moja
aliwahi kuandika kitabu kiitwacho “Refutation to the Religion of
Muhammad (Kuikanusha Dini ya Muhammad)”, ambacho ndio
msingi wa waandishi wengine waliofuata katika kuipinga dini ya
Kiislamu. Waandishi hawa, hawakujua ukweli wa mambo kuhusu
Uislamu kwa sababu walikuwa hawana ujuzi wa lugha ya Kiarabu,
na hali vitabu vya historia ya Kiislamu na Vitabu Vitakatifu
vilivyopatikana katika zama hizo viliandikwa kwa Kiarabu.
Kwa hiyo, haikuwa ajabu kwa Waandishi hao kuandika maandishi
ya kumpinga Mtume wa Uislamu na kumuambia kuwa alikuwa
na tamaa ya wanawake kwa sababu ati alioa wanawake wengi
ambapo Waislamu wengine waliruhusiwa kuoa wanawake wanne tu.
(Waandishi hao walisahau kwamba waandishi wa Biblia la siku hizi
wamewashtaki Manabii wao kwa kuwa na tamaa ya zinaa!).
Hakika, kwa kutowaeleza ukweli ndugu zao Wakristo, na
kumsingizia Mtume wa Islamu (s.a.w.w.) waandishi hao walitumainia
kuyasimamisha maendeleo ya haraka ya kuenea kwa dini ya
3
Kiislamu. Lakini mbinu hizi hazikusaidia vizuri. Tunawaona
wanachuoni wa Kikristo wenye busara wakimtetea Mtume (s.a.w.w.)
dhidi ya masingizio hayo kwa kuyahanusha.
Bila shaka hadithi hizi za masingizio kwa mtume (s.a.w.w.)
hazikubaliwi hata kidogo na Waislamu, kwa sababu sehemu ya
imani yao ni kuiamini “Ismat” (Utakatifu au kutokosea) ya Mitume
(s.a.w.w.).
Wakatii huo huo ni muhimu (kwetu sisi Waislamu) uwafahamisha
wale wasio Waislamu ukweli wa mambo.

 • Jumuiya ya Dar-Rahe-Haq Qum, Iran
 • 2000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 2001
 • Toleo la Nne
 • Dar es Salaam, Tanzania