Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. Malezi Ya Watoto katika Uislamu

Malezi Ya Watoto katika Uislamu

Malezi Ya Watoto katika Uislamu

 • Jopo la Maulamaa (Misri)
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu ulichonacho mikononi mwako asili yake kimeandikwa kwa
Kiingereza na jopo la maulamaa wa Misri kwa jina la Child Care in Islam.
Sisi tumekiita, Malezi ya Watoto katika Uislamu.
Kama inavyofahamika kwamba Uislamu ni dini na ni mfumo wa maisha,
basi mafundisho yake hayakuacha kitu kinachohusiana na maisha ya
mwanadamu – kuanzia tumboni mwa mama yake, kuzaliwa kwake, kunyonya
na kulikizwa kwake, kufunzwa mambo ya kimsingi na mama yake,
mpaka kufikia kimo cha kwenda shuleni. Haya yameelezwa kwa utaratibu
mzuri sana kutoka kwenye vyanzo viwili vikubwa vya sheria ya
Kiislamu – Qur’ani na Sunna.
Kwa mujibu wa Uislamu kipindi cha mafunzo ya watoto huanza wakati
mwanaume na mwanamke wanapoingia katika ushirika wa ndoa, kama
wazazi wa baadaye, ni lazima wajihisi kwamba wana wajibu wa kuwalea
watoto wao. Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa kanuni za kurithi (tabia),
mwenendo wote wa tabia nzuri na mbaya wa wazazi hurithiwa na watoto
wa wazazi hao. Hivyo, mzazi akiwa na tabia nzuri atawarithisha watoto
wake tabia hiyo, na ni kwa sababu hii mafunzo ya watoto huanzia punde tu
wakati mume na mke wanapoingia katika ndoa.
Ili kufanikisha somo la kitabu hiki, jopo hilo la maulamaa limerejea sana
kwenye vyanzo hivyo viwili – Qur’ani na Sunna. Watoto ni taifa la kesho,
na ili kuwa na taifa zuri lenye maadili mema, lazima kuwalea watoto katika
mazingira mazuri ya kimaadili; na ni mafunzo ya Kiislamu tu, kama
yatafundishwa vizuri na kuzingatiwa basi Umma utaondokana na matatizo

mengi ya kijamii kama inavyoonekana hivi sasa.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan katika wakati huu
ambapo jamii inazidi kudidimia katika maovu kutokana na kumomonyoka
kwa maadili mema. Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua
kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale
ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu A. Mohamed kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi
kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa
njia moja au nyingine hadi kufanikisha uchapishaji kitabu hiki.

 • Jopo la Maulamaa (Misri)
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania