Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. MAWAHHABI NA WAUAJI WA IMAMU HUSAIN (A.S.)

MAWAHHABI NA WAUAJI WA IMAMU HUSAIN (A.S.)

 • ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI
 • 2000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

UTANGULIZI
Mara kwa mara baadhi ya watu wajinga husema kuwa wauaji
wa Imamu Husayn (a.s.) walikuwa ni Mashia. Ingawa uongo
huo umekwisha kukomeshwa tangu zamani kwa thibitisho
zisizopingika, bado uongo huu ungali ukitembezwa huko na
huko, ili kwenda kuitambua hoja hii yenye nguvu, na kuweza
kutofautisha baina ya ukweli na uongo, tutatoa hapa hakika tatu
zitakazoongezea kwenye uamuzi usiopingika. Hakika hizi ni:
1.  Ni madhehebu ipi yenye kumheshimu na kumfuata Imamu
Husayn (a.s.) na ni madhehebu ipi yenye kumpinga?
2.  Ni madhehebu ipi inayofikiria kuwa ni wajibu kumlaani
Yazid na ni ipi yenye kumtii (au kwa ujumla kutomtakia
laana Yazid)?
3.  Ni madhehebu ipi inayosikitishwa na kujitenga na maamiri-jeshi wa majeshi ya Yazid yaliyomwua Imamu Husayn (a.s.)
na ni ipi yenye kuwatukuza maamiri-jeshi hao na kuwafikiria
kuwa ni viongozi wa kidini?
Kweli hizi tatu zitatusaidia katika kuwatambua wale
wanaomshutumu na kumkana Yazid na Wafuasi wake wa
kisiasa na wale wenye kuwatukuza na kumchukulia Yazid kuwa
ni Khalifa apasikaye kutiiwa.

 • ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI
 • 2000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 1996
 • Toleo la Kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania