Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. MEZA YA UCHUNGUZI

MEZA YA UCHUNGUZI

 • OmarJumaa mayunga
 • 10000
 • Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Sheikh Umar Juma Mayunga alikwenda Kenya ambako baada ya
mazungumzo ya kidini, alishauriwa na Sheikh Abdallah Nasser
(wa Nairobi) na Haji Ali Muhammad Jaffer (wa Mombasa) kuwa
atakaporudi Dar es Salaam aonane nami kwa maelezo zaidi.
Alikuja kuonana nami, na swali lake la kwanza lilikuwa juu ya
Taqiyah. Nilimpa jibu lililomtosheleza kutoka kwenye Qur’ani
Tukufu na Ahadithi.
Baada ya hapo alikuwa akinitembelea mara kwa mara na mambo
yote aliyokuwa akiyaelewa vibaya (kutokana na propaganda za
kiovu za Wahabiyyah) aliyaelewa vipasikavyo.
Baada ya hapo aliyachambua matukio ya mwenye wakati wa
mwisho wa maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mara tu
baada vitabu muhimu vya historia ya Kiislam kama vile Taarikh
at-Tabari, Taarikh al-Kamil na Sirah Ibn Hisham; Sura
zihusikanazo na historia za vitabu vya Ahadith kama vile Sahih
Bukhari, Sahih Muslim, Kanzul Ummal, n.k.
Baada ya kujifunza matukio hayo, alijifunza vitabu vya Kishia; na
akavutiwa na ukweli wauzungumzao Shia.
Tangu hapo, amekuwa akizitembelea sehemu nyingi za Tanzania
na Kenya. Huko Mombasa alitoa hotuba juu ya Ndoa ya Mut’a na
baada ya hapo aliandika juu ya mada hiyo na kikachapishwa.
Hivi hapa, ili kuusherekea mwaka wa 1400 wa Tukio la Ghadiir-
Khum, amekiandika kitabu ulichokishika. Nimekicheki kitabu
2
hiki na ninathibitisha kwamba rejea zilizotajwa kitabuni humu na
tafsiri zao ni sahihi.
Ninamwomba Allah Subhanahu wa Taala Akijaalie kitabu hiki
kuwa njia ya hidaya kwa ajili ya watu na Amjaalie mwandishi
wake Tawfiiq zaidi kuihudumia dini ya Mwenyezi Mungu kama
inavyofundishwa mwenye Qur’an na Ahlul Bayt (a.s.).
Iwapo msomaji yeyote yule atataka kujua zaidi juu ya jambo
lolote lile lililotajwa kitabuni humu, anakaribishwa kumwandikia
mwandishi huyu ambaye anwani yake imo kitabuni humu.

 • OmarJumaa mayunga
 • 10000
 • Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
 • Dar es Salaam, Tanzania