Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. MKUSANYIKO WA SIFA NA TAREHE ZA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.), IMAMU ALI, BIBI FATIMAH, IMAMU HASSAN NA IMAMU HUSSEIN

MKUSANYIKO WA SIFA NA TAREHE ZA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.), IMAMU ALI, BIBI FATIMAH, IMAMU HASSAN NA IMAMU HUSSEIN

 • AHMAD BADAWY BIN MUHAMMAD AL-HUSSEINY
 • 9976 956 48 7
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye
Kurehemu. Kila sifa njema na shukrani ni za Mwenyezi Mungu,
Mola wa Ulimwengu. Rehema na amani zimshukie Mtume
Muhammad, Jamaa (Aali) zake, na Sahaba zake.
Marhum Sheikh Abdullah Saleh Farsy amefanya kazi kubwa juu ya
Uislamu kwa kutunga MAISHA YA NABII MUHAMMAD (s.a.w.w.
– Sallallahu Alaihi wa Aalihi wa sallam). Ni muhimu sana kwa kila
Mwislamu kukijua kitabu hiki, kwa sababu kimekusanya tarehe na
sifa za Mtume Muhammad (s.a.w.w.).
Kadhalika, Marhum Sheikh Muhammad Kasim Mazrui amefuatisha
vitabu juu ya Makhalifa wanne, baada ya Mtume (s.a.w.w.), navyo ni:
1) Maisha ya Abubakar Asiddik, 2) Maisha ya Umar Al-Faruk,
3) Maisha ya Uthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib.
Vitabu hivi vinne ni muhimu sana na nafuu kubwa kwa Waislamu
wa Afrika Mashariki, kwa sababu vinaeleza kwa Kiswahili tarehe ya
Uislamu baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.).
Ninawahimiza sana Waislamu, wakubwa na watoto, wavisome
vitabu hivyo vitano. Mungu awalipe malipo mazuri Marhum Sheikh
Abdullah Saleh Farsy na Marhum Sheikh Muahammad Kasim
Mazrui, na vizazi vyao, Ninamwomba duniani na Akhera – Amen.
Mimi nimeona vizuri nifuatishe vitabu hivyo kwa kutunga kitabu
juu ya tarehe ya AHLUL-BAYT (Watu wa Nyumbani mwa
Mtume (s.a.w.w.)) na nikakipa jina la AHLUL-KISAA (Watu wa
Kishamia). Sikutaja tarehe ya watoto wote wa Mtume, wala tarehe ya
Wake zake, (Radhiallahu Anhum Ajmaeen – R.A.A.) lakini nimetaja
tarehe za wale tu walioingizwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w.)
2
mwenye KISAA, nao ni Fatimah, Ali, Hassan na Hussein (Alaihimus
Salaam – A.S).
Makusudio yangu ni kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, ambaye
alimwambia Mtume wake awaambie Waislamu: “…. Sema (ewe
Rasuli Wetu Muhammad); Kwa haya (huku kukubalighishieni
Ujumbe wa Allah) sikuombeni ujira wowote, ila mapenzi (yenu)
kwa jamaa (zangu)……..” (Ash-Shuura, 42:23)
Namwomba kila atakayeona makosa katika kitabu hiki, asahihishe
na anipe habari, kwani asiyekosa ni Mwenyezi Mungu tu.

 • AHMAD BADAWY BIN MUHAMMAD AL-HUSSEINY
 • 9976 956 48 7
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 2003
 • Chapa ya Tatu
 • Dar es Salaam Tanzania