Kiislamu vyanzo

  1. home

  2. book

  3. MTUME WA AMANI SAYYIDINA MUHAMMAD Al-MUSTAFA (S.a.w.w.)

MTUME WA AMANI SAYYIDINA MUHAMMAD Al-MUSTAFA (S.a.w.w.)

  • Sayyid Ali Naqi Saheb
Rate this post
description book specs comment

Shukurani zote ni zake Yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t.), rehma na
amani zimshukie Mtukufu Mtume na Aali zake wote.
Kwa vile cheo cha Uislamu katika historia ya ulimwengu siyo cha
kidini tu, bali cha kitamaduni na cha siasa pia, upo umuhimu
mkubwa na manufaa makubwa katika kujifunza maisha ya
Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa mataifa na ustaarabu wa kila
mwanadamu. Zaidi ya hayo, kuisoma historia ya Mtume
Muhammad (s.a.w.w.) ni faradhi na wajibu kwa kila Muislamu.
Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ameleta na kufundisha mambo
mengi sana kwa ulimwengu huu. Qur’an Tukufu aliyoileta kutoka
kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni kielelezo bora cha utukufu wake.
Miongoni mwa faida zilizopatikana kutokana na mwangaza wa
Qur’an Tukufu, ni mwamko wa kujitegemea, kisiasa, kiuchumi,
kijamii na kinadharia.
Wale wasiomjua Mtume Muhammad (s.a.w.w) na wayasome
maisha yake na historia yake kwa ujumla. Wanaweza pia kuelewa
cheo chake watakapoisoma Qur’an Tukufu. Mtume Muhammad
(s.a.w.w) ni Mtume wa Mungu katika msururu mrefu wa Mitume
na yeye ndiye mwisho wa Mitume, kwa maana hii hatakuja wala
hapatatokea Mtume yeyote yule atokaye kwa Mwenyezi Mungu.
Ni matumaini yangu kuwa kijitabu hiki kitawafurahisha mno
Waislamu.

  • Sayyid Ali Naqi Saheb