Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. MUHAMMAD (S.A.W.W) NI NABII WA MWISHO

MUHAMMAD (S.A.W.W) NI NABII WA MWISHO

 • Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 2004
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

“SAUTI YA BILAL”, ni Gazeti la Kiswahi litolewalo na “Bilal Muslim
Mission of Tanzania”, kwa ujumla limetambulikana kama gazeti
lipashalo habari zaidi na lenye maelezo mengi zaidi ya dini katika
Afrika ya Mashariki nzima. Mnamo mwaka 1968, Misheni hii ilitoa
maelezo kuhusu suala la “Khatme-Nubuwwah” (mwishilizo wa
Unabii) katika makala tatu zilizotolewa katika matoleo matatu
mfululizo. Si ajabu kuwa mfululizo huo ulipokewa kwa mikono miwili
na wasomaji wote Waislamu.
Suala la kuwa Muhammad (s.a.w.w), Mtume Mtukufu wa Uislamu,
alikuwa Mtume wa Mwisho, na kwamba hakuna atakayepata Utume
baada yake, ilikuwa ni imani rahisi, lakini imani kubwa ya kila
Mwislamu. Misheni ilieleza imani hii ya Kiislamu katika maandishi
hayo ya Kiswahili, ikinakili Aya za Qur’ani tukufu na Hadithi za Mtume
(s.a.w.w) toka vitabu mbali mbali vya waandishi wa Hadithi za Mtume.
Mhubiri mmoja wa Kiqadiani aliandika barua ndefu ya Kiswahili
akijaribu kuyapinga maandishi hayo. Barua hii ilijibiwa na Allamah
Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Chief Missionary. Kwa kuwa hapakuwa
na jibu toka kwa mhubiri huyo, hakukuwa na usemi zaidi. Hata hivyo,
mwanafunzi mmoja wa Kishia mwenye asili ya Kiafrika baadaye
alimwandikia barua Maulana akiomba uthibitisho wa imani ya
“Khatme-Nubuwwah”. Katika barua hiyo vifungu fulani fulani
vilionekana kuwa na uhusiano mkubwa na barua ya yule mhubiri wa
Kiqadiani. Ni wazi kuwa Maqadiani walikuwa wakitawanya barua yao
bila ya kujali makanusho aliyoyatoa Allamah Sayyid Saeed Akhtar
Rizvi. Hivyo Misheni haikuwa na njia nyingine ila ile ya kutawanya
jibu la Maulana ambalo lilikuwa na kurasa ishirini na nne za karatasi
ndefu zilizorudufiwa. Nakala moja ilipelekwa kwa mwanafunzi huyo,
ambaye baadaye alileta barua ya kueleza jinsi alivyotosheka kabisa na
jibu hilo.
3
Matukio hayo yalitolewa katika “Bilal News” kama kawaida; na Haji
Hasanally P. Ebrahim (wa Karachi) aliomba nakala chache. Kwa kuwa
habari hizo ziliandikwa kwa Kiswahili, Maulana kwa hisani yake
alikubali na aliahidi kuzitafsiri kwa Kiingereza kwa faida ya watu wengi
zaidi. Wakati huo nilimuomba Maulana aongeze mambo fulani fulani
ili kuikamilisha zaidi kazi hii. Namshukuru Maulana kwa kulikubali
ombi langu hilo.
Kitabu hiki ni matokeo ya juhudi yake Allamah Sayyid Saeed Akhtar
Rizvi istahiliyo sifa, na habari nyingi zihusuzo Khatme-Nubuwwah
zimezungumziwa kwa kirefu. Vile vile kitabu hiki hutuonyesha jinsi
fikra za Maqadiani zilivyo.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu akikubalie kitabu hiki na ambariki
Maulana.
Asgherali M. M. Jaffer

 • Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 2004
 • Toleo la Kumi
 • DAR ES SALAAM TANZANIA