Kiislamu vyanzo

  1. home

  2. book

  3. MUT’A NDOA SAHIHI

MUT’A NDOA SAHIHI

  • OmarJumaa mayunga
download

    Download

5 (100%) 1 vote[s]
description book specs comment

Alhamdulillahi, kila sifa njema ni ya Mwenyeezi Mungu, Bwana
wa walimwengu. Na Rehma na Amani zimshukie Bwana wetu na
Muombezi wetu Muhammad S.A.W., na ziwashukie Aali zake
watakatifu, na wanaofuata na kuusimamia uongozi wao mpaka siku
ya mwisho.
Ndoa ya Mut’a ni katika mas’ala waliyokhitilafiana Shia na Sunni
kutoka mwishomwisho wa utawala wa Khalifa wa pili (Umar bunul
Khattab) mpaka leo. Tarehe 17/8/1988 kwa tarehe 3 Muharram 1408
katika ukumbi wa Bilal house, Mombasa, nilizungumza juu ya ndoa
ya Mut’a.
Tarehe 1/9/1989 katika Msikiti wa Al’azhar Mombasa, Sheikh
Muhammad Sharif Famau alinijibu. Sheikh alizungumzia mambo
matano:-(a) Uadilifu wa Masahaba.
(b) Tahriful Quran.
(c) Wilayatu Ali A.S.
(d) Taqiyya.
(e) Ndoa ya Mut’a.
Mimi katika kitabu hiki nitashughulika na Mut’a, na haya mengine
yameshaanza kujibiwa na Mzee wangu Sheikh Abdilahi Nassir. Kwa
hivyo, yeyote anayependa kujua majibu ya vifungu hivyo atasoma
vitabu vya Sheikh Abdilahi vya majibu hayo.
Sheikh Muhammad Sharif katika darsa yake alizungumzia kwamba:-(a) Mut’a ilikuwako wakati wa Mtume.
(b) Kisha Mtume aliiondoa kabla ya yeye kufa.
0
ii
(c) Kwa hivyo hivi sasa Mut’a ni haramu yeyote anayeoa hivyo
ANAZINI.
Kwa mtazamo wa Sheikh Muhammad Sharif Mut’a ni Zina, na
ametoa hoja zake.
Kwa hakika, nachukua nafasi hii kumpa pongezi za kweli
kabisa. Ndugu yangu Sheikh Muhammad Sharif Famau kwa hatua
aliyochukua ya kusahihisha lile ambalo anaona linapotoshwa nje
ya misingi ya Islam. Huu ndio msimamo wa Islam, na mwislamu
anapaswa kuwa hivi.
Sisi tuko tayari kujadili Qadhia ya Mut’a kwa ukamilifu, lakini kwa
sharti:
(a) Hatutaki matukano wala kejeli.
(b) Tuzungumze kielimu.
Kwa hivyo sisi tunaonyesha:-(a) Mut’a ilikuwako wakati wa Mtume,
(b) Mtume S.A.W. hakuiondoa mpaka amekufa.
(c) Kwa hivyo ndoa hii si haramu, ni halali mpaka siku ya mwisho.
Kuthibitisha hayo, kutalazimu kuvunja hoja za Sheikh Muhammad
Sharif, na kutoa dalili za kuthibitisha kuwa iko, kutokana na vitabu
vinavyokubaliwa na Sunni wote.
Mwenyeezi Mngu atupe TAWFIQ, Ee Mola! Tuonyeshe Haki
tuifahamu kuwa ni Haki uturuzuku kuifuata. Na tuonyeshe batili
tuifahamu kuwa ni batili uturuzuku kuiepuka.

  • OmarJumaa mayunga