Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. MUT’A NDOA YA HALALI

MUT’A NDOA YA HALALI

 • Abdilahi Nassir
 • 2003
 • Chapa ya Kwanza
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Bwana wa viumbe vyote. Na
swala na salamu zimshukie Mtume Wake, Muhammad, pamoja na aali
zake waliotwahirishwa wakatwahirika, na wote wenye kufuata nyayo zao
mpaka Siku ya Mwisho.
Hiki ni kitabu juu ya mut’aambayo, kwa ufupi, ni ndoa ambayo
kwayo mwanamke, kwa kuridhiana na kukubaliana na mwanamume
atakayemuowa, hujioza kwa mahari maalumu na kwa muda maalumu
– bora tu iwe hapana kizuizi chochote cha kisharia cha kuzuiya ndoa
hiyo kufanyika. Muda huo unapokwisha, ndoa hiyo nayo hwisha pasi na
kuhitajia talaka.
Kuwa ndoa hii ilikuwako zama za Mtume Muhammad s.a.w.w., na
kuwa iliruhusiwa na yeye mwenyewe, ni jambo linalokubaliwa na
Waislamu wote kwa itilaki. Lisilokubaliwa ni: jee, baada ya kuruhusiwa,
ndoa hiyo iliachwa kuendelea au ilifutwa (mansukh)? Hapa ndipo palipo
na makindano.
Kuna wanaoshikilia kuwa ndoa hii haikufutwa bali iliachwa kuendelea
na kuruhusiwa hadi hii leo; kwa hivyo ni halali. Hao ni mashia. Kuna
wanaokataa hilo: wanaodai kuwa ilifutwa na hairuhusiwi tena: kwa hivyo
ni haramu. Hao ni masunni.
Katika kitabu hiki nia yangu ni kuthubutisha si kwamba ndoa hii ilikuwa
halali zama za Mtume Muhammad s.a.w.w. tu, bali ingali halali hadi hii
leo kinyume cha madai ya wanaoipinga. Inshallah nitafanya hivyo kwa
ushahidi wa vitabu vya wao hao wanaopinga. Na kuwafikiwa ni kwa
Mwenyezi Mungu

 • Abdilahi Nassir
 • 2003
 • Chapa ya Kwanza