Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. MWENGE WA HAKI

MWENGE WA HAKI

 • 5000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 1987
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu hiki ni tafsiri ya mazungumzo kati
ya Khalifa mashuhuri wa Kiislamu aitwaye
Ma’mun Ar-Rashid na wanachuoni arobaini
wa Kiislamu wenye elimu ya juu kabisa wa
zama hizo. Jambo walilojadiliana ni ubora
wa Sayyidana Ali bin Abi Talib (a.s.) juu
ya Masahaba wengine wa Mtume Mtukufu
(s.a.w.w.).
Mazungumzo hayo yameandikwa na Bw.
Abu Umar Ahmad bin Mohammad bin
Abdi Rabbih Al-Undulusi (246 A.H. – 327
A.H) katika kitabu chake mashuhuri Al
Iqdul-Fareed. Mwanachuoni huyu Bw. Ibnu
Abdi Rabbih alikuwa mashuhuri sana, na
alikuwa mwenye elimu ya Lugha na alikuwa
mtunga mashairi pia. Tangu hapo zama-ni watu walitambua na kujua thamani na
kutunuka kwa kitabu chake hicho, hata
wakawa wanapenda mno hata walijifunga
kwa kukitalii na kudondoa mule na
2
wakazitumia katika kutungia vitabu vyao
na kuzungumzia katika hutuba zao. Na
kilipigwa chapa mara nyingi sana kuanzia
waka 1292 A.H. hadi 1384 A.H. miaka sita
mbele.
Nakala tunayo katika Maktaba yetu hapo
Dar-es-salaam, imepigwa chapa Cairo
(Misri) katika mwaka 1384 A.H (1965 A.D)
baada ya kuangaliwa na kusahihishwa na
wanachuoni watatu.
Mazungumzo hayo yameandikwa katika
juzu ya tano, kuanzia uk. 92 hadi uk.101,
chini ya anwani:
هنع للہا ضیر علی لضف فی ءاھقفلا علی نوماملا جاجتلحا
(Majadiliano ya Ma’mun na Wanachuoni
kuhusu ubora wa Ali R.A).

 • 5000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 1987
 • Toleo ya Tatu
 • Dar es Salaam - Tanzania