Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. MWISLAMU KATIKA NJIA PANDA

MWISLAMU KATIKA NJIA PANDA

 • Ayatullah Muhammad Baqir al-Sadr (a.r.)
 • 3000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Tunamshukuru Allah (s.w.t.) na kwa Baraka za Mtukufu Mtume
(s.a.w.w.) na Watukufu Ahlul-Bait (a.s.) kwa kutujalia kuweza
kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapisha kitabu hiki “Mwislamu
katika njia panda”.
Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya Makala mbili
(zilizo tarjumiwa kutoka kiingereza) kutoka kwenye kitabu “Ghadir”
zinawasilishwa hapa kwa faida ya wasomaji wetu wa Kiswahili.
Tarjuma ya kwanza ya Ash-shahidi Ayatullah Muhammad Baqir
al-Sadr mwanzo ilichapishwa kutoka kwenye kitabu “A study on the
question of Al Wilaya” (Uchunguzi juu ya swala la Al Wilaya) katika
lugha ya kiingereza.
Anuani “Mwislamu Katika Njia Panda” imechaguliwa kwa ajili ya
kijitabu hiki kuelezea tukio kubwa la kihistoria lilitokea Ghadir Khum
katika al-Juhfa ambako njia za watu wa Madina, Misri na watu wa Iraq
zinakutana.
Hapa, binamu mashuhuri na mkwe wa mtukufu Mtume Ali bin Abi
Talib alitangazwa na mtukufu Mtume mwenyewe kama “Maula”
1
(Walii Amr) wa Waislamu wote.
Siku yenyewe ilikuwa Alhamisi ya Zilhijja 18. Hapa mtukufu Mtume
alisimamisha msafara wa zaidi ya watu laki moja kuwatangazia
“Wilaya”
2
ya Imamu Ali bin Abu Talib.
Ni matumaini yetu kwamba wasomaji watanufaika kutokana na yale
yanayowasilishwa bila upendeleo na waandishi katika makala hizi.

Maombi yetu kwa Allah (s.w.t.) ni kwa Waislamu wote wanawake na
wanaume katika nyakati hizi ngumu.
Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale wote
ambaye kwa juhudi zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu
mikononi na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au
nyingine katika uchapishaji wa kitabu hiki, Tunamuomba Allah (s.w.t.)
awalipe malipo mema hapo Duniani na baadaye huko, Akhera.

 • Ayatullah Muhammad Baqir al-Sadr (a.r.)
 • 3000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 2005
 • Toleo la Kwanza
 • Dar es Salaam - Tanzania