Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. Ndoa KatiKa Islam

Ndoa KatiKa Islam

 • Amiraly M. H. Datoo
 • 2500
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Zipo riwaya nyingi mno ambazo zimenakiliwa kutoka Mtume
s.a.w.w. na Maimamu a.s. ambazo zinasema kuwa mwenye kuoa
anakuwa amejidhibiti vyema katika Islam na nusu ya sehemu ya
imani inambidi afanye jitihada ili aweze kuiimarisha. Mwenye kuoa,
rakaambili za mwenye kuoa ni afadhali kuliko rakaa sabini za mtu
asiyeoa. Aliyeoa ni mpenzi wa Allah s.w.t.
Mtume s.a.w.w. amesema kuwa mtu asifanye uchelewesho katika
kuoa kwani watoto watakaozaliwa watakuwa wakimtii na kumtukuza
Allah s.w.t. ambapo ujira wake utakuwa ukipatiwa wazazi wao na
mema yao pia yatakuwa yakilipwa wao. Vile vile amesema kuwa
tuuendeleze Ummah wake ili aweze kuwa na fakhari Siku ya Qiyama.
Iwapo mwanamke mimba yake itaanguka basi Siku ya Qiyama mtoto
wake huyo atakataa kuingia Jannat (Peponi) hadi hapo wazazi wake
waingizwe nae pamoja. Limetolewa onyo kuwa “kufa bila ya kuoa ni
vibaya mno.”
Imam Jafar as-Sadiq a.s. amenakiliwa akisema kuwa “Iwapo
nitakuwa na dunia pamoja na vitu vyake vyote vikawa vyangu bila
ya kupitisha usiku mmoja bila mwanamke, basi mimi siridhii hayo
yote. Ni afadhali kukosa vyote hivyo kuliko kukosa mwanamke. Vile
vile sala ya aliyeoa ni afadhali kuliko sala za kila siku pamoja na
saumu za asiyeoa.”
Vile vile kuna riwaya isemayo kuwa mtu atakapo kujitakasa mbele
ya Allah swt, basi inambidi afanye harusi na kuoa katika hali ya
umasikini na ufukara ni kuthibitisha imani na uaminifu juu ya Allah
s.w.t. kwani Allah s.w.t. amesema “Oeni hata katika hali ya umasikini
na ufukara kwani nitawaghaniisha.”
Ipo katika riwaya kuwa muoe wake wazuri na mtu atakayeoa
mwanamke kwa sababu ya tamaa ya mali au uzuri, basi atakosa
vyote. Na atakayeoa kwa kuangalia dini na imani ya mwanamke,
basi atapata mali na uzuri vyote.
Katika kumsifu mwanamke, ni bora kuliko dhahabu na fedha na
mwanamke mwovu ni mbaya sana kwani hata mchanga ni afadhali
kuliko yeye. Mwanamke mwenye gharama ndogo na vilevile
anazaa watoto kwa urahisi na mwanamke mwenye mahari ndogo
basi ni mwema na mwanamke mwenye gharama kubwa na mwenye
kuzaa watoto kwa mushkeli na mwenye mahari kubwa, basi
mwanamke kama huyo si mwema.
Ni Sunnah kusoma nikah wakati wa usiku, kwani Allah s.w.t.
ameufanya usiku kuwa mapumziko na starehe na inapoangukia
Qamar dar Aqrab(nyota iwapo katika Nge) basi msifanya
nikah na kunapokuwa joto kali, iwapo kutakuwapo na ndoa, basi
kunauwezekano wa kuachana. Vile vile kusifanywe ndoa siku ya
jumatatu kwani siku hiyo ni mbaya mno na iwapo itakuwa ni siku
ya kuzaliwa kwa Ma’sum a.s. au Idd basi hakuna shida yoyote.
Haifai kuoa katika tarehe 26, 28 na 30 za kila mwezi.
Kuoa si faradhi lakini iwapo kuna hatari ya kutumbukia katika
maasi, basi itakuwa ni faradhi kuoa, na kwa mjane kolewa si vibaya,
kwani kubakia pekee mara nyingi inakuwa mushkeli kimaisha na
hivyo haitakiwi kujitumbukiza katika magumu ya maisha ambapo
tunaweza kujiepusha. Kwa hakika ni jambo la kusikitisha kuona
katika jamii yetu wajane wakitupwa bila kujali na kudharauliwa
kama ni wenye nuksi ambapo inatubidi sisi kuwajali na kuwatunza
na kuwaoza inapowezekana ili wao nao waweze kuishi maisha kama
wengineo wote.
Ipo Hadith inayosisitiza mno kabisa kumfanyia na kumgharamia
mtu harusi na nikah kwani inayo thawabu adhimu. Kila neno
litakalosemwa na kila tendo litakalotendwa na kila hatua
itakayochukuliwa, Allah swt atampa thawabu za sala za usiku na
saumu za mwaka mzima. Na huko Jannat atampatia Hur al-Ainelfu
moja wakiwa na majumba yaliyorembeshwa kwa Yaqutina vito vya
thamani.
Ipo riwaya inayosema kuwa atakayemwozesha mjane, basi Siku ya
Qiyama atakuwa miongoni mwa wale waliorehemiwa na Allah swt.
Atakaye suluhisha baina ya bibi na bwana, basi Allah swt atamjaalia
thawabu za mashahidi elfu na hatua zozote zile atakazozichukua
katika kufanyisha suluh na matamshi yote yatakayotoka atapatiwa
thawabu za ibada za mwaka mzima.

 • Amiraly M. H. Datoo
 • 2500
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 1996
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam - Tanzania