Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. NYAMA YA NGURUWE

NYAMA YA NGURUWE

 • Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
 • 2000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kijitabu hiki, kilichoandikwa kwa mpango wa
mazungumzo kuhusu Nyama ya Nguruwe,
kiliandikwa na Sayyid Saeed Akhtar Rizvi. Sayyid
Saeed Akhtar Rizvi ni Mwanachuoni na Mtafiti
wa Kiislamu. Vile vile ameandika vitabu vingi juu
ya Uislamu ambavyo vinatolewa na Jumuiya hii
ya “Bilal Muslim Mission of Tanzania.”
Katika kijitabu hiki, mwandishi amepinga vikali
sana kuhusu kula Nyama ya Nguruwe, akitoa
sababu za kisayansi na za kidini, ili kulithibitisha
jambo hili, ametumia ripoti za kiganga na za
kijamii ambazo zinathibitisha wazi wazi bila ya
kubakisha shaka yoyote ile juu ya athari mbaya
za Nyama ya Nguruwe kwa afya na uadilifu wa
mwanadamu.
Kwa vile kijitabu hiki tumekiona kuwa kinafaa
3
mno hapa ketu Afrika ya Mashariki kwa
kuondoa fikara mbaya walizonazo ndugu zetu
wasio Waislamu kuhusu Sheria ya Kiislamu juu
ya mnyama huyu nguruwe, tumeona kuwa ni
bora tukitafsiri kwa lugha ya Kiswahili ili kiweze
kuwasaidia hata wale ndugu zetu ambao
hawakujaaliwa kuielewa lugha ya Kiingereza.
Mwishoni tunamwomba Mwenyezi Mungu atupe
sisi Waislamu mafanikio mema hapa duniani na
Kesho Ahera pia.Tuwe wasikivu wa Neno Lake na
wafuasi wa Uongozi Wake wa Kweli – Amin.

 • Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
 • 2000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 2011
 • Toleo la Tatu
 • Dar es Salaam Tanzania