Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. SHIA NA HADITH MAJIBU NA MAELEZO

SHIA NA HADITH MAJIBU NA MAELEZO

 • Abdilahi Nassir
 • 5000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimshukie bwana
wetu na mwombezi wetu, Muhammad b. Abdillahi, na ali zake wema
waliotakaswa wakatakasika, na wote wanaofuata nyayo zao.
Hiki ni kitabu cha pili katika mfululizo wa majibu yetu ya al-Khututul
Aridhwakilichoandikwa na marehemu Sheikh M. al-Khatib kwa lugha ya
Kiarabu, kiasi cha miaka thelathini iliyopita, na kufasiriwa kwa Kiswahili
huku Kenya, hivi karibuni, kwa jina la Misingi Mikubwa lliyojengewa Dini
ya Ushia.
Katika kitabu hiki, tumejaribu kuyajadili yote yale ambayo Sheikh M. al-Khatib aliyaeleza dhidi ya Shia, kuhusu Hadith za Mtume Muhammad
s.a.w.w. Na kama tulivyofanya katika kitabu chetu cha kwanza, Shia na
Qur’ani, tumeyalinganisha hayo na yale yanayopatikana katika vitabu vya
Kisunni.
Ni matumaini yetu kwamba, baada ya kukisoma kitabu hiki, itakudhihirikia
kwamba hakuna hitilafu kubwa hivyo baina ya msimamo wa Sunni juu
ya Hadith na ule wa ndugu zao, Shia, hata iwazuie wao kukurubiana na
kuelewana kama alivyopendelea Sheikh M. al-Khatib. Kitu cha pekee
kinachozuia ndugu wawili hao kuelewana ni zile chuki zinazojengwa
baina yao na wale ambao watapata hasara lau ndugu hao watasikilizana
na kuungana!
lli uweze kufaidika na majadiliano yaliyomo humu, na yale yaliyomo ka-tika vitabu vyetu vingine katika mfululizo huu, ningependa uhakikishe
kwamba:
i. Unayo nakala ya hicho kitabu cha Sheikh M. al-Khatib tunachokijibu.
Kama huna, jaribu kukipata kutoka mojawapo ya anwani hizi:
S.L.P. 70541; au 67971; au 48509: zote za Nairobi, Kenya.
Hivi vyetu, unaweza kuvipata kwa kutuandikia kwenye S.L.P. 86260,
Mombasa, Kenya.
ii. Tunapotaja kwamba maneno fulani ya Sheikh M. al-Khatib yamo
kwenye ukurasa fulani wa kitabu chake, hakikisha umefungua ukurasa
huo na kuyakinisha kwamba tumeyanukuu maneno haya vilivyo. Kama
sivyo, tafadhali tuandikie utukosoe ili tuweze kujisahihisha. Maana nia
yetu si kumzulia marehemu Sheikh uwongo, bali ni kujenga umoja wa
Waislamu kwa kujaribu kuondoa kutoelewana kulioko baina yao.
iii. Tunapotoa ushahidi wa vitabu fulani, ujaribu kuangalia ushahidi huo
katika vitabu hivyo, kwa lugha unayoielewa. Kama hakuna kwa lugha
hiyo, basi mwendee shekhe yeyote aliye karibu nawe, na ambaye
hayuko upande wowote katika mzozo huu, umwombe akuangalilie
katika nuskha za Kiarabu alizonazo yeye ili uhakikishe kwamba
tulivyo nukuu ndivyo. Kama sivyo tafadhali usisite vile vile kutujulisha
ili tuweze kuelekezana.
Mwisho, ningependa kurudia tena kwamba lengo letu katika kuandika
majibu haya si kutafuta ubishi wala mizozo, bali ni kutaka tu kuonyesha
kwamba vile vikwazo vya kuzuia uelewano na umoja baina ya Sunni na
Shia, ambavyo Sheikh M. al-Khatib alidhania viko, haviko! Kama tutafaulu
kulithibitisha hilo, tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwa maslaha ya
Waislamu wote.

 • Abdilahi Nassir
 • 5000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 2001
 • Toleo la Pili
 • Dar es Salaam - Tanzania