Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. SHIA NA SAHABA MAJIBU NA MAELEZO

SHIA NA SAHABA MAJIBU NA MAELEZO

 • Abdilahi Nassir
 • 5000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimshukie
bwana wetu na mwombezi wetu, Muhammad b. Abdillahi, na ali zake wema
waliotakaswa wakatakasika, na wote wanaofuata nyayo zao.
Hiki ni kitabu cha tatu katika mfululizo wa majibu yetu ya al-Khututul
Aridhwakilichoandikwa na marehemu Sheikh M. al-Khatib kwa lugha ya
Kiarabu, kiasi cha miaka thelathini iliyopita, na kufasiriwa kwa Kiswahili
huku Kenya, hivi karibuni, kwa jina la Misingi Mikubwa iliyojengewa Dini
ya Ushia.
Katika kitabu hiki, tumejaribu kuyajadili yote yale ambayo Sheikh M. al-Khatib aliyaeleza dhidi ya Shia, kuhusu sahaba wa Mtume Muhammad
s.a.w.w.; na kila tulilolijibu na kulieleza, kama desturi yetu, tumelitolea
ushahidi wa vitabu vya Kisunni vyenyewe.
Hata hivyo, ni jambo la kufurahisha kujua kwamba, baada ya majibu yetu
haya kutoka, baadhi ya mashekhe wa Kisunni walitukosoa kwa kusema
kwamba mzozo huu tulionao si baina ya Sunni na Shia, bali ni baina ya
Wahabi na Shia. Na hilo ni kweli. Maana, mbali ya kuwa huyo Sheikh M. al
Khatib mwenyewe alikuwa Wahabi, unapotazama wote wale waliojitokeza
dhidi ya Shia katika mzozo huu unawakuta ni Wahabi vile vile — ima
kwa imani au kwa kulipwa. Pamoja na hayo, katika majibu yetu haya,
tumelazimika kuonekana tunajibizana na Sunni kwa sababu tu Sunni
wenyewe wamemwachia Sheikh M. al-Khatib kutumia jina lao bila ya
kujibari naye. Lau mashekhe wa Kisunni wangalijitokeza na kuwafahamisha
Sunni wenzao hitilafu kubwa iliyoko baina yao na Wahabi, bila shaka ndugu
zetu wa Kisunni wangalielewa ule uadui mkubwa dhidi ya Bwana Mtume
s.a.w.w. na Uislamu kwa jumla, ambao Wahabi wanajaribu kuuficha kwa
kujitokeza kama watetezi wa Usunni. Hilo inshallah ni nia yetu kulifanya,
baada ya kumaliza mfululizo huu, pamoja na kuonyesha ushirikiano
uliokuwako, na ambao ungaliko hadi leo, baina yao na ukoloni wa
Kiingereza dhidi ya masilahi ya Uislamu!
Mara tu baada ya kutoa majibu yetu haya, mmoja kati ya ‘wanafunzi’
wa Sheikh M. al-Khatib alijitolea, katika darasa zake, kujaribu kutujibu.
Kama ameweza kufanya hivyo au la si juu yangu kusema. Ni juu ya wale
wanaohudhuria darasa zake na/au wale waliowahi kuzisikia kanda zake.
Lililo juu yangu ni kusema kuwa, ilipotoka tafsiri ya kitabu cha Sheikh M.
al-Khatib, mimi sikujibu kwa darasa, japokuwa ninazo. Nimeijibu kwa
maandishi vile vile. Kwa hivyo, ili wasomaji wetu wafaidike kwa majibizano
haya, tunangojea majibu ya maandishi* (sio ya mdomo).
Vile vile mmoja kati ya ndugu zetu alijitolea kuandaa majadiliano juu ya
suala hili. Hivyo aliniandikia barua ambazo kwa kuwa, baada ya kutoka,
zimeelezwa visivyo katika baadhi ya vyombo vya habari, na hata
madarasani, nimechukua fursa ya kuzichapisha humu (uk. 49-54) ili
wasomaji wetu wajue ukweli wa mambo ulivyo. Kwa sasa hivi, hadi kitabu
hiki kilipokwenda mitamboni, tumefikia hapo. Inshallah chochote
kitakachotokea baada ya hapo tutakitoa katika vitabu vyetu vijavyo. Na
kuwafikiwa ni kwa Mwenyezi Mungu.

 • Abdilahi Nassir
 • 5000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 2001
 • Toleo la Pili
 • Dar es Salaam - Tanzania