Kiislamu vyanzo

  1. home

  2. book

  3. Sura Al Fatiha (Ufunguzi Wa Kitabu)

Sura Al Fatiha (Ufunguzi Wa Kitabu)

  • Bashir Haiderali Alidina
download

    Download

Rate this post
description book specs comment

Naomba kinga kutokana na shetani aliyelaaniwa, kuanza kwa Jina la Mola Ambaye ameumba, bila yeye Mwenyewe kuumbwa.
Sifa zote zinamstahiki Allah (S.W.T) Ambaye ameiteremsha Qur’an Tukufu juu ya mja Wake mpenzi mno ili kwamba aweze kuwa mbebaji wa habari njema na muonyaji kwenye ulimwengu. Baraka ziwe juu ya Mtukufu Mtume (S.A.W.) na juu ya kizazi chake kitoharifu ambao walitoharishwa kwa utakaso ulio kamili kabisa.
Naomba mwongozo kutoka kwa mola wa ulimwengu ili kuniwezesha kukamilisha jukumu hili kubwa ambalo ninaliingia kabla ya kuondoka kwenda kwenye awamu nyingine ya maisha yangu. Sijifikirii mwenyewe kuwa na uwezo hata wa kuweza kukwaruza uso wa Kitabu kitukufu mno ya vitabu vyote na nitajiona mwenyewe mwenye bahati kama ningekuwa na uwezo wa kufikisha kitu kidogo mno cha mabadiliko ya milele na maana ya Qur’an Tukufu kwa watu wa kawaida katika namna nyepesi ya kutosha kwa kadiri kwamba iwe rahisi kueleweka. Ili kufanikisha hili nitajaribu na kuepusha nyingi ya hoja za kifundi na kifilosofia ambazo huonekana kwa zaidi katika vitabu vikubwa vya tafsir.
Namuomba Allah (S.W.T.) Aliye juu, kunipa umri mrefu wa kutosha kukamilisha tafsir hii na kukubali jaribio langu hili la unyenyekevu mno kuanza kulipa ajr-e-risaalat.
Kwa mara nyigine tena namuomba Allah (S.W.T.) Yeye aliye juu, kuniongoza na kunisaidia kuweka maelezo yangu kwenye lengo. Hakika Yeye ni Msaidizi na Kiongozi bora.

  • Bashir Haiderali Alidina