Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. UHARAMISHO WA KAMARI

UHARAMISHO WA KAMARI

 • Amiraly M. H. Datoo
 • 2000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Ninamshukuru Allah swt pamoja na Mtume Mtukufu s.a.w.w.
na Ahli-Bayt Toharifu a.s. kwa kunijaalia neema hii ya kuweza
kukitarjumu kijitabu hiki juu ya maudhui haya ya kamari ili
kuweza kuwafaidisha wanaadamu wenzetu ili nao waweze kujiokoa
na janga hili kubwa linaloangamiza watu pamoja na famili zao
zikiteseka kizazi baada ya kizazi.
Mimi binafsi nimewaona wajukuu ambao mpaka leo wanateseka
kwa ajili ya madhambi ya mababu zao. Vile vile hapa mjini kwetu
nilikuta watu wenye mapesa wakiongoza katika makundi yao ya
kucheza kamari kwa mapesa, yaani Waislamu ndio waliokuwa
wakiendesha madanguro hayo. Kwa hakika nilijaribu kutoa
makala juu ya uharamisho wa kamari, lakini niliyokumbana nayo
yananitosha, na wala sina haja kuyaelezea hapa. Ndipo hapo
nilipoona umuhimu wa kukitayarisha kijitabu hiki juu ya uovu wa
kamari.
Makusudi yangu ni kutaka kuwasaidia na kuwaelimisha watu juu
ya uovu huo wa kamari.
Ni mategemeo yangu kuwa maudhui haya yatatufaidisha na
kutuongoza katika njia njema yenye kujenga maisha yetu na ya
jamii nzima kwa ujumla.

 • Amiraly M. H. Datoo
 • 2000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 1996
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam - Tanzania