Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. UISLAMU

UISLAMU

 • Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
 • 1000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
download

  Download

2 (40%) 1 vote[s]
description book specs comment

Pengine Madhehebu ya Kiislamu ya Shia Ithna-ashariyah, ndio
Madhehebu isiyofahamika sana miongoni mwa ndugu zetu wasio-Mashia na wasio-Waislamu pia. Imetokea hivi kwa sababu ya uchache
wa maandishi ya Kiingereza yazungumziayo juu ya Madhehebu hii.
Mwislamu wa siku hizi anaelekea sana kwenye kuusoma Uislamu kwa
Lugha ya Kiingereza au lugha nyingineyo ya kienyeji. Watu hawajali
sana wala hawapendelei kujifunza Lugha za Kiarabu na Kiajemi
(Kiirani), lugha zenye vitabu vya asili na vyenye elimu za Madhehebu
ya Shia Ithna-ashariyah.
Hivi sasa Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Sheikh mkazi wa
Jamaat ya Shia Ithna-ashariyah ya mjini Dar es Salaam amekubali
kuandika kitabu kutokana na hotuba yake aliyoitoa kuhusu Ushia, na
pia amekubali kuifanyia masahihisho hotuba hiyo na kuweka maelezo
zaidi katika sehemu zote zihitajizo kufanyiwa hivyo. Maulana aliitoa
Hotuba hii kwenye Chuo Kikuu cha Makerere kilichoko mjini
Kampala, nchini Uganda, na baadae akaitoa tena mjini Moshi,
nchini Tanzania, mbele ya Wanavyuoni wa dini mbali mbali wenye
elimu ya juu. Haina haja kusema hapa kwamba wanavyuoni hao
waliufurahia mfuatano wa maarifa wenye kutegemeana na urahisi
wa kufahamika, vitu ambavyo Maulana alivitumia katika kuyaeleza
maelezo ya mafundisho ya awali kabisa ya Uislamu, kama
yanavyofundishwa katika Madhehebu ya Shia Ithna-ashariyah.
Halmashauri yangu inategemea kwamba kitabu hiki kitampa
mwanafunzi yeyote ajifunzaye dini za siku hizi, taarifa ya kutosha juu
ya Madhehebu ya Shia Ithna-ashariyah; na vile vile kitampa msomaji
wa kawaida nuru itoshelezayo kuhusu Madhehebu hii — Insha Allah.

 • Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
 • 1000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 2007
 • Chapa ya Tano
 • Dar es Salaam Tanzania