Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. UJUMBE SEHEMU YA PILI

UJUMBE SEHEMU YA PILI

UJUMBE SEHEMU YA PILI

 • Sheikh Ja’far Subhani
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza
kiitwacho, The Message, kilichoandikwa na Sheikh Ja’far Subhani. Sisi
tumekiita, Ujumbe. Kwa vile kitabu hiki ni kikubwa, tumekigawa katika
juzuu nne ili kuwarahisishia wasomaji wetu kukisoma kwa makini katika
kila sehemu. Hii uliyonayo mkononi ni Juzuu ya Pili.
Kitabu hiki kilichoandikwa na mwanachuoni mkubwa Sheikh Ja’far
Subhani kimekuwa ni miongoni mwa vitabu bora vilivyofanya utafiti wa
kina kuhusu historia ya Uislamu na Waislamu.
Haya ni matokea ya utafiti wa kielimu pamoja na hoja zenye nguvu na
utumiaji sahihi wa akili uliofanywa na mwanachuoni mwandishi wa kitabu
hiki juu ya maudhui haya yaliyotaja hapo juu.
Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo
makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na
upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za
watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua
kuchapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake
yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa
Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii.
Tunamshukuru ndugu yetu, Maalim Dhikiri Kiondo (Allah ‘Azza wa Jalla
amkubalie amali zake na amweke karibu na Maasumina 14 [a.s.] – Amin)
kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile
tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi
kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

 • Sheikh Ja’far Subhani
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania