Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. UJUMBE WA IMAM KHOMEINI KWENYE MAADHIMISHO YA MILENIA YA NAHJU ’l-BAlÃGHAH

UJUMBE WA IMAM KHOMEINI KWENYE MAADHIMISHO YA MILENIA YA NAHJU ’l-BAlÃGHAH

 • Imãm Sayyid Rouhullah Khomeini
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • Dar-es-Salaam Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kijitabu hiki kimebeba ujumbe wa Ayatullah al-Uzma Imãm Khomeini (Mwenyezi Mungu ampe
daraja la juu Peponi), muasisi wa Mapinduzi
ya Kiislamu ya Iran; Ujumbe alioupeleka
kwenye Mkutano wa kusherehekea kupita miaka
elfu moja ya mtungo ya Nahju ’l-Balaghah,
uliofanyika mjini Tehran mwezi Mei, 1981.
Ujumbe huu, licha ya ufupi wake unavuta
hisia katika nyanja nyingi za kitabu; hisia
ambazo zinalenga katika masuala ya Kidini,
Irfani, Falsafa, Maadili, Elimu, Jamii, Ulinzi,
Utamaduni na zinginezo.
Mkusanyaji wa Nahju ’l-Balaghah, as-Sayyid
ash-Sharif ar-Radhi (359 – 406 A.H.) ameuweka
Ulimwengu wa Kiislamu chinni ya ufadhili
wake kwa kuweka katika mikono yao Kioo
ambacho wataona taswira halisi ya Mzungumzaji
na Mwandishi wa Hotba, barua na Hadithi hizi
ambaye ni Kiongozi wa Waumini ‘Ali ibn Abi
Talib (a.s.).
Hivi sasa Mheshimiwa Kiongozi wa Kitengo cha
Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran, kushirikiana na Bilal Muslim Mission
of Tanzania na Ahlul~Bayt (a.s.) Assembly of
Tanzania wanachapisha tafsiri ya Kiswahili ya
Ujumbe huo kwa ajili ya Semina ya Nahju ’l-Balaghah itakayofanyika Dar-es-Salaam tarehe
28 na 29 Septemba, 2001, kwa lengo la jamii
izungumzayo Kiswahili kupata nafasi ya
kuzingatia kutafakari kuhusu ujumbe huu
muhimu wa Imãm Khomeini (R.A.) na kupata
mwongozo kutokana nao.

 • Imãm Sayyid Rouhullah Khomeini
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • Dar-es-Salaam Tanzania