Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. UKWELI ULIOPOTEA 5

UKWELI ULIOPOTEA 5

 • Shaikh Mu’tasim Sayyid Ahmad
 • 1000
 • Alitrah Foundation
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu
kiitwacho al-Haqiqatu ‘dh-Dha’i’ah kilichoandikwa na Sheikh Mu’tasim
Sayyid Ahmad. Sisi tumekiita, Ukweli Uliopotea. Kwa vile kitabu hiki ni
kikubwa, sisi tumekigawa katika juzuu tano ili kiwe chepesi kusomwa na
wasomaji wetu wa Kiswahili. Hiki ulichonacho mkononi mwako ni juzuu
ya kwanza.
Kitabu hiki ni utafiti uliofanywa na mwanachuoni huyo wa Kiislamu
kuhusu madhehebu za Kiislamu. Utafiti wake huu ulihusisha pia maho-jiano na mijadala baina yake na na masheikh wa Kiwahabi na maustadh
wake katika chuo alikosoma.
Kama kawaida katika utafiti wake, ametumia sana vitabu vya historia ya
Kiislamu na vya hadithi vilivyoondikwa na wanavyuoni wa Sunni na Shia,
kisha akahitimisha kwa Qur’ani Tukufu na Sunna. Baadhi ya vitabu hivyo
ameviorodhesha ndani ya kitabu hiki ili msomaji aweze kuvirejelea. Lakini
bahati mbaya sana mengi ya matoleo mapya ya vitabu hivyo yamefanyiwa
mabadiliko na baadhi ya sehemu kuondolewa, hususan zile zinazounga
mkono madai ya Shia. Ufuatao hapa chini ni mfano mdogo tu wa yanay-ofanywa katika vitabu hivyo:
Katika ukurasa wa 301 wa juzuu ya 3 ya Tafsir al-Kashshaafiliyokusany-wa chini ya maelekezo ya Sheikh Mustafa al-Halabi (toleo la pili, 1319
A.H. liliochapishwa na Main Government Printing House ya Amiriah
Bulaq ya Misri), beti zinazojitokeza ambazo kwazo Jarallah Zamakhshari,
mfasiri wa al-Kashshaaf,alitangaza wazi imani yake katika uhalali wa
Ushia. Lakini katika toleo la mwaka wa 1373 A.H. kutoka Printing House
Istiqamah bi ‘l-Qahara, shairi lililotajwa halionekani tena.
Marehemu Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi katika kitabu chake kiitwa-cho, Uimamu,ukurasa wa 37, anaandika kushangazwa kwake kutokana
na maneno yaliyoondolewa katika kitabu cha at-Tarikhat-Tabari,chapa ya
Leiden (ya mwaka 1879 Miladia). Chapa hii ya Leiden imeyanakili
maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) aliyoyatumia wakati wa karamu
mashuhuri ya ndugu wa karibu aliyoitayarisha ambapo katika khutba yake
alisema: “Enyi watu wangu! Huyu Ali ni ndugu yangu, Wasii wangu na
Khalifa wangu miongoni mwenu; msikilizeni na mtiini.” Lakini katika
chapa ya Misri ya mwaka 1963, (chapa inayodaiwa kuwa imechekiwa na
ile ya Leiden) maneno haya muhimu: “Wasii wangu na Khalifa wangu”
yamebadilishwa na kuandikwa “kadha wa kadha” na kusomeka hivi:
“Huyu Ali ni ndugu yangu na kadha wa kadha.” Huu ni msiba mkubwa.
Huu ni mchezo umefanywa na unaendelea kufanywa mpaka leo. Na lengo
ni kuficha ukweli. Lakini hata hivyo, ‘ukweli siku zote unaelea’; matoleo
ya zamani yapo mengi na yamehifadhiwa kwenye maktaba zetu.
Ni muhimu kufikia kila aina ya maoni katika kujaribu kuamua ukweli.
Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa. Utafiti huu umefanywa
ili kuwaelemisha Waislamu kwa ujumla juu ya madhehebu za Kiislamu ili
kujenga maoni yao kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe, na ni
muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao. Inawezekana
kusemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni
tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu (mtazamo) wa kwao wenyewe.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa
maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano
za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena
katika akili za watu.
Kutokana na ukweli huo, taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua
kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake
yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa
Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Harun Pingili kwa kukubali jukumu
hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote
walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa
kwake.

 • Shaikh Mu’tasim Sayyid Ahmad
 • 1000
 • Alitrah Foundation
 • Juni, 2010
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania