Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. “ULUL AMR” NI NANI?

“ULUL AMR” NI NANI?

 • Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
 • 2000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
download

  Download

2 (40%) 1 vote[s]
description book specs comment

Waislamu wamegawanyika makundi wawili
kuhusu maana ya maneno “Ulul-Amr”
yaliyotumika katika Aya ya 59 ya Surat
An-Nisa.
Wako wasemao kuwa maana ya maneno
haya ni “Watawala kutoka miongoni mwenu”
– yaani watawala wa Kiislamu; na hii ndio
tafsiri ifuatwayo na Waislamu walio wengi
(Masunni).
Wako wengine wasemao kuwa, maana ya
maneno hayo ni “Makhalifa (au Maimamu)
Maasumiin (Watakatifu) Walioteuliwa na
Allah kushika mahali pa Mtukufu Mtume
(s.a.w.a) baada ya yeye Mtume (s.a.w.a)
kuondoka”. Hii ndio tafsiri ifuatwayo na
Mashia-lthna-ashariyah.
Kutoafikiana huku ni tatizo lihitajilo kutatuliwa
kwa njia fulani. Kwa vile msingi mkuu
wa Uislamu ni kutumia akili, inatulazimu
kuutumia, msingi huu huu katika suala hili.
Maneno yafuatayo ni maelezo ya Ndugu
yetu Sayyid Saeed Akhtar Rizvi aliye Mhubiri
Mkuu wa Misheni yetu, akijaribu kulitatua
tatizo hili kwa njia hii ya kutumia akili
na kwa kuzichunguza aya nyingine za
Qur’ani. Tunategemea kuwa, Insha-Allah
wewe msomaji wetu nawe utafaidika kutokana
na kijitabu hiki.
Mwisho tunamwomba Allah atujaalie Tawfiq
katika kuyasoma maneno Yake na kupata
maana yake halisi itakayotuongozea kwenye
Mwongozo wake halisi – Amin.

 • Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
 • 2000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 1986
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam -Tanzania