Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. UPENDO KATIKA UKRISTO NA UISLAMU

UPENDO KATIKA UKRISTO NA UISLAMU

UPENDO KATIKA UKRISTO NA UISLAMU

 • Mahnaz Heydarpoor
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Maudhui iliyoshughulikiwa katika kitabu hiki ni ya umuhimu mkubwa
sana. Inataka kuonesha vipi upendo ulivyo katika moyo wa kiroho na
maadili ya imani mbili kubwa, kati kati yake ambapo kujuana kukubwa na
kufahamiana baina ya imani hizi mbili kunahitajika kwa haraka mno
iwezekanavyo.
Uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu umepatwa na athari ya urithi wa
historia wa mashaka na chuki inayojitokeza katika nyakati ambapo falme
zenye nguvu na ustaarabu ulioshirikishwa nazo, wamejikuta wenyewe
katika mizozo na mapambano. Ushindi wa Waislamu wa rasi ya Iberia, vita
vya msalaba, kuanguka kwa Constantinople, nia ya ukubwa wa dola ya
Ottoman na ubeberu wa magharibi wa karne ya 19 na ya 20, yote haya
yameacha mabaki ya machungu na uadui. Hii imeendelea leo kujidhihirisha
yenyewe katika Mashariki ya Kati, katika Balkan na katika sehemu
mbali mbali za ulimwengu. Katika jamii za magharibi taarifa za vyombo
vya habari juu ya harakati za vurugu za Waislamu wanaowaita wa siasa
kali au imani kali vimeelekea pasina haki kabisa, kuhusisha Uislamu na
Waislamu na ushabiki wa dini ambao kwa kiasi kikubwa umeondolewa
katika upendo. Ni kana kwamba ule uhusiano kati ya Wakatoliki na
Waprotestanti katika Northern Ireland ni wa kuwakilisha uhalisi wa
Ukiristo.
Pamoja na mambo haya ya kusikitisha, kuna vipengele zaidi mno vya historia
ambavyo ni bayana vya uhusiano kati ya imani hizi mbili na ustaarabu
wao. Ni rahisi mno kusahau miundo mingi ya elimu ya wote pamoja na
utajiri wa utamaduni walioshirikiana katika sanaa, usanifu majengo,
filosofia, hisabati, sayansi, na fasihi kwa karne nyingi.
Maeneo ya mapatano ya kiteolojia kati yao (na vile vile na uyahudi),
yamekuwa vile vile yanafahamika kwa kiasi kidogo sana. Wana
kukubaliana kwa sawa sawa kuhusu ufunuo wa vitabu vya dini na simulizi
za kiutume za imani hizi mbili; uthibitisho wa pamoja wa imani katika
Mungu wa Ibrahim; na msisitizo mkali juu ya umuhimu wa kumtukuza
Mungu katika ibada na kuishi maisha katika njia iliyoelekezwa na sheria
Zake. Kufanana na mwingiliano wa fikra na kiroho wa baadhi ya walimu
wakubwa na ma-irifani wakati wa kipindi cha karne za kati huonekana vile
vile kusahauliwa kabisa.
Hata hivyo, katika kubadilisha maadili ya kijamii ya mfumo wa misimamo
mingi zaidi ya kidini, hali ya uungaji mkono ya ukoloni katika nchi za
magharibi, na hisia kubwa ya jumuiya ya ulimengu mzima (utandawazi)
iliyoletwa na mawasiliano bora, kwa haraka misimamo inageuka.
Mazungumzo kati ya imani za dini na utashi wa kutafuta ujuzi wa kweli,
kuachwa huru kutoka chapa za zamani na za kisasa, kumejitokeza zaidi
mno katika nchi za magharibi, shukurani kwa kazi za wanachuoni kama
vile John Esposito na Ninian Smart. Ingawa kukua kwa jumuiya za
Kiislamu katika jamii za watu wa Ulaya hakukuwa bila matatizo na
migogoro, utashi mkubwa unajitokeza miongni mwa kizazi cha vijana ili
kuweka hali ya baadaye ya pamoja iliyosimama juu ya kuheshimiana na
kujifunza imani na utamaduni kutoka kwa kila mmojawao.
Ni kwa ajili ya moyo huu kwamba kitabu hiki kimeandikwa. Kwa
mtazamo wa matatizo mazito ambayo yamejitokeza kati ya Iran, U.S.A na
U.K. kwa miongo miwili iliyopita, haya yote ni ya muhimu zaidi kwamba
kitabu hiki ni cha mwanachuo kijana, Shia wa Iran, Mahnaz Heydarpoor.
Mhitimu wa Chuo Kikuu mashuhuri cha Qum, ambaye alikuja Uingereza
na mumewe na familia yake katika mwaka wa 1997, mara tu alionesha
kuvutiwa katika kuchukua mafunzo zaidi na utafiti. Imekuwa ni furaha
kubwa kwangu kuwa msimamizi wake na kukutana na wote, Mahnaz na
mumewe Mohammad Shomali, ambaye yeye mwenyewe ni mwanachuoni
mwenye kuheshimika. Wote wamekuwa mabalozi wazuri kwa Iran na kwa
Uislamu na nimejfunza mengi kutoka kwao kuhusu tabia na moyo wa
Uislamu kisha kutokana na kusoma vitabu vingi.
Shauku ya Mahnaz ya kuamua kuongeza ujuzi wake wa Ukiristo na juhudi
na nguvu ambazo kwazo amefuatilia lengo lake hili, sio tu kwa kusoma
vitabu, bali pia kwa kukutana na Wakristo wa usuli za madhehebu mbali
mbali na vikundi kama vile Chama cha Focolare, imekuwa ya kuvutia
mno. Uchanganuzi wake juu ya upendo katika Ukiristo ni wa kisomi na wa
utambuzi mno, lakini itakuwa ni ufafanuzi wake wa ukuu wa upendo katika
teolojia ya Kiislamu na maadili ambao hususan utakuwa wa kuvutia
kwa wasomaji wa Magharibi, Wakristo na wengineo.
Inatumainiwa kwamba ari ya Mahnaz itaweza kulipwa na wasomi wengi,
kama yeye wanaotafuta maeneo ya mazungumzo ili kuzidisha tathmini ya
wote na ujuzi kati ya Uislamu na Ukiristo. Vile vile inatumainiwa kwamba
ukunjufu na ukarimu wa kiroho (kwa neno, upendo wake) vile vile utalipwa,
ili kwamba uponaji wa vidonda vya huzuni vilivyosababishwa na
chuki ya karne nyingi na kutokuelewana kunaweza kuharakishwa kwa
faida ya mamilioni.

 • Mahnaz Heydarpoor
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania