Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. UTOKEZO (AL-BADAA)

UTOKEZO (AL-BADAA)

 • Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani
 • 1000
 • AL-ITRAH FOUNDATION
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabu
kiitwacho, al-Badaa’.Sisi tumekiita, Utokezo.
Kitabu hiki ni matokeo ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni
wa Kiislamu, Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani.
Kumekuwepo na kutokuafikiana katika miji yetu ya Kiislamu, hususan
miongoni mwa wanavyuoni kuhusu usahihi wa itikadi ya Badaa’ – yaani
utokezo wa jambo fulani kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Baadhi wanase-ma kwamba itikadi hii ni sahihi na wengine wanasema si sahihi. Baadhi ya
wanavyuoni wamekwenda mbali zaidi hadi kufikia kuwaita Waislamu
wenzao wanaoitakidi juu ya Utokezo (Badaa’) kuwa ni washirikina au
makafiri.
Lakini je, Badaa’ haina asili katika dini? Ukweli ni kwamba ina asili kati-ka dini kama utakavyoona katika kitabu hiki.
Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo
makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na
upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za
watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imea-mua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni
yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa
Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii.
Tunamshukuru ndugu yetu, Abdul-Karim J. Nkusui kwa kukubali jukumu
hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote
walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa
kwake.

 • Sayyid Abdul-Karim al-Bahbahani
 • 1000
 • AL-ITRAH FOUNDATION
 • 2009
 • Toleo la kwanza
 • Dar es Salaam, Tanzania