Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. VISA VYA WACHAMUNGU

VISA VYA WACHAMUNGU

 • Shahid Ayatullah Murtadha Mutahhari
 • Alitrah Foundation
 • Julai, 2010
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha
Kiingereza kiitwacho, Anecdotes of Pious Menkilichoandikwa na
Shahid Ayatullah Murtadha Mutahhari. Sisi tumekiita, Visa vya
Wachamungu.
Kitabu hiki ni mkusanyiko wa visa vya kweli vya wachamungu
mbalimbali wa Kiislamu. Visa hivi vimefika kwetu kama viigizo na
mafundisho kwa waumini ili nao angalao wapate kufikia kiwango
cha uchamungu wa kweli. Ndani ya kitabu hiki mna visa ambavyo
huweza kuhuisha nyoyo za waumini, na iwapo vitazingatiwa sawa-sawa, vitamfanya muumini kufanya ibada zake kwa usahihi na kuji-amini.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu
wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na
ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua
kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni
yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji
wa Kiswahili.
Tuwamshukuru ndugu zetu, Hussein Hassan na Rajab Osman kwa
kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile
tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine
hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.
Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto
kubwa kwa wasomaji wetu.

 • Shahid Ayatullah Murtadha Mutahhari
 • Alitrah Foundation
 • Julai, 2010
 • Toleo la kwanza