Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Muhammad (a.s.)

Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Muhammad (a.s.)

 • MOHAMMED RAZA DUNGERSI, Ph.D.
 • 1000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Hatimaye, Kwa Rehema za Allah, nimekamilisha kuandika wasifu
huu mfupi wa Imamu wetu wa kumi, Imam Ali Naqi (a.s.) kwa ajili ya
wasomaji wale ambao wanahitaji kupata mukhtasari wa maisha ya Imam
huyu aliyeteuliwa kimungu.
Kuna taarifa nyingi mno juu maisha ya Imam wetu wa kumi kiasi
kwamba katika hatua za mwanzo nilikuwa sina dalili ya wapi pa
kuanzia na wapi pa kumalizia jukumu hili la kutisha ambalo nimekubali
kulifanya kwa niaba ya Bilal Muslim Mission of Tanzania. Jinsi
ninavyozidi kufikiria kuhusu mradi huu, ndivyo ninavyozidi kuhisi
kuvunjika moyo, mpaka wakati nilipogundua kwamba kulikuwepo na
watu wachache waliosoma wasifu fupi nilizoandika juu ya Maimam
wengine, na ambao walikuwa wanaulizia kutoka Bilal Muslim Mission
wapewe maelezo ya kwa nini sikuandika juu ya maisha ya Maimam
wetu wa kumi, wa kumi na moja na wa kumi na mbili. Kuuliza huku
kwa mara nyingine tena kulinipa moyo zaidi kujikusanya na kutumia
nguvu zangu kwenye jukumu hili ambalo halijakamilika. Matokeo ya
juhudi hii ni mukhtasari huu mfupi unaolezea maisha ya Imam wa
kumi, Hazrat Ali Naqi (a.s.).
Kila mara ninapopitia kazi hii wakati ikiwa bado katika muundo wa
muswada, nilikuwa naona kwamba bado ilikuwa haifai kuchapishwa
kwa vile haikufikia hata mambo muhimu ya msingi ya haiba ya mtu
huyu maarufu. Niliishia kwa kufanya marekebisho mengi mno.
Hatimaye, nilifikia hitimisho kwamba kama nitafuata silka yangu,
kamwe kazi hii haitamalizika. Kwa hiyo sasa tunayo kazi hii fupi kwa
ajili ya wasomaji wangu. Maombi yangu kwa Muumba ni kwamba
Anisamehe kwa mapungufu ambayo huenda yamebakia bila kuonekana
katika kitabu hiki.
Nachukua fursa hii kuwashukuru wote wale ambao kwa njia moja au
nyingine wamenisaidia katika juhudi zangu za kufanya na kukamilisha
jukumu hili. Shukurani zangu maalumu za moyoni ni kwa ajili ya
Mzee Fidahusein Abdullah Hameer, Mchapishaji, ambaye alivumilia
kukawia kwangu na huku mara kwa mara akinikumbusha jukumu langu
la kukamisha kazi hii.

 • MOHAMMED RAZA DUNGERSI, Ph.D.
 • 1000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 2012
 • Toleo la Kwanza
 • Dar es Salaam - Tanzania