Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Musa (a.S.)

Wasifu mfupi wa Imam Ali bin Musa (a.S.)

 • MOHAMMED RAZA DUNGERSI, Ph.D
 • 1000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Mwishoni mwa miaka za 50 na mapema miaka za 60, wakati
nilipokuwa mwanafunzi wa Madrasa katika shule ya Faize
Zanzibar, kulikuwa hakuna somo kama la Historia ya Kiislamu
katika mitaala ya Madrasa. Kwa hiyo, wakati nilipojiunga na kikosi
cha kufundisha cha Husseini Madrasah mjini Dar es Salaam,
Tanzania mapema katika miaka za 80, na hatimaye nikateuliwa
kufundisha somo la Historia ya Kiislamu, nilichanganyikiwa
nikiwa sijui ni kitu gani nifundishe.
Sio tu kwamba kulikuwa hakuna mtaala kwa ajili ya somo hili. Bali,
wajibu wangu mkubwa ulikuwa ni upeo wa mtaala wenyewe. Kwani
kwenye kiini cha Mtaala wa Historia ya Kiislamu ilikuwa kujifunza
maisha ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wale MASOOMIN kumi
na tatu wengine ambao wanaotokana na kizazi chake.
Kwa mtazamo wangu, mbali na kitabu bora cha Yusuf Laljee KNOW
YOUR ISLAM (UJUE UISLAMU WAKO), kulikuwa hakuna kita-bu kingine rahisi bali hata maandiko ya kielimu ambayo yanaweza
kutumiwa kwa kujitosheleza kwa wote, walimu na wanafunzi kwa
usawa. Hata hivyo, sehemu ya historia ya maisha ya MASOOMIN
ilikuwa sio kamili katika kitabu KNOW YOUR ISLAM.
Kuanzia siku hizo, nilihisi haja ya kukusanya kwa ufupi mukhtasari
wa kufundishia juu ya maisha ya Maimam wetu kumi na mbili
(a.s.) pamoja na malengo mawili akilini. Kwanza, kuangalia katika
maeneo yote yale ya habari, bila kuacha taarifa za kihistoria,
ambazo zitamuwezesha mwanafunzi kuelewa hali changamani
ambayo kwayo Maimam wetu wameishi na kutekeleza majukumu
yao kama wateule viongozi wa kiungu wa ulimwengu. Pili,
kuwasilisha taarifa hii katika mtindo ambao una kiini chake
cha masilahi, hali kadhalika na uwezo ulio sawa wa walimu na
wanafunzi. Niliona jukumu hili ni rahisi kuingia akilini lakini
gumu sana kulitekeleza. Ni wazi kwamba, ningeweza kukamilisha
kidogo katika eneo hili mpaka wakati nilipohamia Marekani.
Kwa bahati mbaya au nzuri, katika Husseini Madrasah wa New
York, kwa mara nyingine tena niliteuliwa kufundisha Historia
ya Kiislamu. Kwa sababu ambazo sihitaji kuzieleza hapa, niliona
jukumu hili la kutisha mno kuliko ilivyokuwa katika Afrika.
Kwa bahati nzuri, katika wakati huu mgumu wakati nikiwa
napapasa gizani nikitafuta maandiko bora ya kufundishia kwa ajili
ya darasa langu, niliteuliwa na by Maulana Sayyid Saeed Akhtar
Rizvi, Mhubiri Mkuu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania,
kuandika vijitabu vya kufundishia vinavyohusisha maisha ya
Maimam wetu 12 (a.s.) kwa ajili ya Masomo kwa Njia ya Posta
yanayoendeshwa na Bilal Mission. Kwangu mimi hii ilikuwa
neema ya Allah iliyoletwa katika njia mbili:
Kwanza, uteuzi huu ulinipa moyo na imani ambayo nimeikosa
mpaka sasa. Sasa ninao msaada wa mmoja wa mwanachuoni
maarufu wa Shia wa zama yetu hii – Sayyid Saeed Akhtar Rizvi.
Pili, sitakuwa na wasiwasi kuhusu kutafuta mfadhili kwa ajili
ya uchapishaji na usambazaji wa maandishi yangu; Bilal Muslim
Mission of Tanzania italifanya hilo.
Kwa hiyo, kijitabu hiki na vyingine vitakavyokuja ni matokeo ya ari
na msaada kamili wa Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, utawala
wa Bilal Muslim Mission of Tanzania mwenyekiti wake wa zamani
Al-haj Fidahusein Abdullah Hameer.
Yote, mada, hali kadhalika na mtindo wa kijitabu hiki (na vingine
vifuatavyo) vimefanywa vyepesi kueleweka, ili kuafikiana na
ushauri wa Maulana Sayyid Saeed Akhtar kwamba “Lazima
tuzingatie kwamba vijitabu hivi vya masomo vimekusudiwa kwa
vijana na sio kwa wanachuoni.”
Yote yamesemwa na kufanywa, licha ya tahadhari ya hali ya juu
zilizochukuliwa ili kukifanya kijitabu hiki kuondokana na kasoro
na makosa mengine. Hata hivyo, kama baadhi yamebakia bila
kusahihishwa, mimi ndiye muwajibikaji.
Allah anisamehe kwa makosa haya ambayo hayakukusudiwa na
awalipe wale wote ambao wamenisaidia kwa njia moja au nyingine
katika kuandika, uchapishaji na usambazaji wa kijiatabu hiki.

 • MOHAMMED RAZA DUNGERSI, Ph.D
 • 1000
 • BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
 • 2012
 • Toleo la Kwanza
 • DAR ES SALAAM - TANZANIA