Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. Wasifu mfupi wa Imam Husayn (a.s.)

Wasifu mfupi wa Imam Husayn (a.s.)

 • MOHAMMED RAZA DUNGERSI, Ph.D.
 • 1000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Haya yalikuwa ni matakwa ya Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
kwa miaka kadhaa sasa, kujumuisha wasifa za Maasumeen
14 katika Masomo yetu ya Kimataifa kwa njia ya Posta, lakini
kutokana na shughuli zake kuwa nyingi ulimwenguni pote
ilimzuiya kulitekeleza jukumu hili.
Bilal Muslim Mission of Tanzania inamshukuru sana
Dr. Mohammed Raza M. Dungersi wa New York ambaye
amejitolewa kulitekeleza jukumu hili gumu na la kutisha.
Hakuna mwanahistoria au mwandishi yoyote, kwa umahiri
wowote atakaokuwa nao, awezaye kutoa picha ya kweli ya maisha
ya Maasumeen (a.s.). Hata hivyo, tunampongeza Dr. Dungersi kwa
juhudi hii kubwa na kumuomba Allah amlipe malipo mema hapa
duniani na kesho Akhera.
Maisha ya watu wa kubwa hutukumbusha jinsi ya kufanya
maisha yetu kuwa na msukumo. Historia ya watu wakubwa ni
chemchemi ya elimu, imani na ari amabyo kamwe haitakauka.
Maisha ya watu hawa ni kama nyumba za mwanga, ambazo
huondoa giza na kuonesha njia iliyonyooka kwa wasafiri
wanaotafuta elimu, maisha bora na huduma kwa wanadamu.
Lau kama watu hawa wakubwa wasingeacha nyayo juu ya mchanga
wa zama, ulimwengu ungekuwa unapapasa gizani na ungeangukia
kuwa mawindo kwenye ukataji tamaa wakati ambapo unapambana
na nguvu na akili zisizoonekana.
Hili ni chapisho la tatu katika mfululizo wa mradi huu mkubwa
ambao chini ya mfululizo huu wa vijitabu hivi linakwenda
kuchapishwa. Dr. Dungersi tayari amakamilisha wasifu wa
Maimam wetu wanne wa mwanzo.

 • MOHAMMED RAZA DUNGERSI, Ph.D.
 • 1000
 • Bilal Muslim Mission of Tanzania
 • 2012
 • Toleo la Kwanza
 • DAR ES SALAAM - TANZANIA