Kiislamu vyanzo

 1. home

 2. book

 3. YAZID HAKUWA AMIRUL-MU’MININ

YAZID HAKUWA AMIRUL-MU’MININ

 • Abdilahi Nassir
 • Bilal Muslim Mission of Kenya
 • Mombasa - Kenya
download

  Download

Rate this post
description book specs comment

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu; na swala na salamu zimshukie
Mtume Wake pamoja na aali zake waliotwahirishwa; amin.
Mwanzo mwanzo wa mwezi wa Muharram wa mwaka huu (1424 BH),
palitolewa karatasi katika mji wa Mombasa zenye kichwa cha habari
“Barua ya wazi kwa wahubiri na maimamu wa sunna” (uk. 30 humu).
Lengo la karatasi hizo lilikuwa ni kuwaonyesha hao wahubiri na
maimamu wa kisunni makosa wanayoyafanya ya kuweka “vikao
vya mawaidha, khususan katika siku kumi za mwanzo wa mwezi wa
Muharram”. Kwa maoni ya waandishi wa karatasi hizo, “hakuna hadith
(dalili) ambayo inatuambia tufanye hivyo” isipokuwa huo ni “uzushi”
ambao, kwa kuufanya, “mwawapoteza wafuasi wa Sunna kwa kuwaiga
hao hao Ma-Shia”.
Waliozitoa karatasi hizo walijiita “Ahlul-Tawheed” ambao, kama
wasomi wote wanavyojua, ni mawahabi. Wao hutumia jina hilo kwa
sababu mbili. Sababu ya kwanza ni kuficha uwahabi wao wanaojua
kwamba unapingwa na Waislamu wote. Kwa hivyo wanaogopa kukosa
kuungwa mkono. Sababu ya pili ni kutokana na ile imani yao kwamba
wao peke yaondio wanaompwekesha Mwenyezi Mungu; Waislamu
wengine wote wasiokubaliana nao, kwao wao, ni mushrikina. Lakini
kwa kuwa Waislamu wotewanaamini kwamba wao ni ahlut tawhiid,
kwa vile wotewanaikiri Laa ilaaha illallaah, waandishi wa karatasi hizo,
kwa kutumia jina hilo, walitaka kuwavungavunga Waislamu wawafikirie
kuwa ni wenzao.
Ili kuzijibu tuhuma walizozifanya dhidi ya mashia kuhusu mauaji ya
Imam Hussein (a.s.), na ili kuyasahihisha madai waliyoyafanya katika
karatasi zao, kuwa Yazid alikuwa Amirul-Mu’minin, nilitoa mfululizo
wa karatasi kumi, kuanzia tarehe 8 Muharram 1424 / 12 Machi 2003
hadi 14 Rabii-ul-Awwal 1424 / 16 Mei 2003, nilizozipa kichwa cha habari
“Barua ya wazi kwa mawahabi.” Karatasi hizo ndizo hizi tulizozikusanya
katika kitabu hiki. Na kuwafikiwa ni kwa Mwenyezi Mungu.

 • Abdilahi Nassir
 • Bilal Muslim Mission of Kenya
 • Mombasa - Kenya